Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj akizngumza na wajumbe wa mkutano huo
Akizngumza wakati
akifungua mkutano mkuu wa bodi ya wanachama wanaokutana jijini Dar es salaam
kwa lengo la kupitisha majina ya wagombea urais wa chama hicho,mwenyekiti wa
chama hicho cha ADC Mhe. Said Mirajamesema kuwa kwa hali ilivyo sasa uchaguzi unaokuja mwezi wa kumi
utakuwa kati ya ccm na ccm wenyewe huku upinzani ukiwa hauna nguvu kutokana na
kuwapikea baadhi ya makada wa chama chama mapinduzi na kuwapa dhamana kubwa
ndani ya vyama hivyo.
Mwenyekiti
wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj Akisalimiana na mlezi wa chama hicho
ambaye sasa ndiye mgombea wa urais
zanzibar kwa tiketi ya chama hicho
wakisalimiana wakati wa
ufumnguzi wa mkutano huo
Wakati macho na maskio
ya watania yakiwa yanaangalia mnyukano wa kisiasa unaoendelea nchini baina ya
chama cha mapinduzi na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA nacho chama kipya
kinachokuja kwa kasi chama cha ADC wameibuka na kusema kitendo kilichofanywa na
vyama vya upinzani kuwachukua baadhi ya viongozi wa chama tawala na kuwapa
madaraka ni muendelezo wa kuwasaliti watanzania na kuendelea kuipa nafasi CCM .
Wajumbe wakiwa katika mkutano huo
Amesema kuwa kwa hali
inayoendelea sasa nchini Tanzania ni wazi kuwa hakuna mtanzania aliye na nia ya
dhati ya kuwasaidia watanzania ila ni ADC pekee kwa kuwa wao hawako tayari
kuwapokea makada wa chama chochote waliokatwa na kuwapa madaraka kwani nao ndio
wanaweza kuwarudisha watanzania tena kule ambapo wanakupinga.
Kauli hii inakuja ikiwa
waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mh EDWARD LOWASA amekihama chama chake na
kuhamia cha cha democrasia na maendeleo chadema huku makada kadhaa wa chama
hicho wakiendelea kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani.