Dar es salaam
Sisi kama
Uongozi wa Masjid Ghadir, sisi kama Uongozi wa Chuo cha Imam Swadiq vilivyopo
Kigogo Post Dar es salaam, vilevile sisi kama Viongozi, Maimam katika Madhehebu
ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.
Tunawatakia
Watanzania wote kwa Ujumla, pasina kujali dini zao, pasina kujali madhehebu
zao, tunawatakiwa kheri ya Eid, tusheherekee Eid hii kama wafuasi wa Dini
tofauti tukiwa na sifa nzuri ambazo anazipenda mwenyezimungu (swt).
Katika
kuipokea Eid napenda niiseme falsafa kubwa ya fungu anayoizungumzia
mwenyezimungu ndani ya Qur’an, anaema malengomakubwa ya funga ili watu wawe
wachamungu,ndio falsafa kubwa ya funga.
Sasa funga
yetu hii ya mwaka huu ya 2017, funga hii itupelekee watanzania wale tuliofunga
kuwa wachamungu, na nitaongea sifa tano kwa harakaharaka ambazo sifa hizi ni
sifa za mchamungu.
Sifa ya
kwanza ya jamii inayomcha mungu wanakuwa na mapenzi yaani wanapendana, kwahiyo
funga yetu tulioifunga kwa mwaka huu iwe ni chachu ya watanzania wale
waliofunga na wale ambao hawakufunga iwe ni chachu na sababu ya wao
kupendana.Iwe ni sababu ya wao kushikamana, iwe ni sababu ya wao kuelewana.
Watanzania
waislamu na wasiokuwa waislamu Wakristo na Madhehebu mengine watakapo pendana,
watakapo shikamana, watakapo kuwa kitu kimoja, watajaribu kuondoa matatizo
mengi yaliyopo katika jamii yao.
Katika
matatizo hayo watajitahidi kuhakikisha ufakiri, Umasikini unasambaratika katika
jamii yaliyomo, kwa sababu waswahili wanasema seku zote kwamba kidole kimoja
hakivunji chawa, kwa hivyo mapenzi yao baina yao, mapenzi yao, mshikamano
utasababisha wapambane waondoe ufakiri, umoja wao utasababisha wapate suluhisho la wajane tuliokuwanao
Tanzania.
Umoja wao na
mapenzi yao utasababisha watafute suluhisho na dawa ya mayatima, vilevile
watatafuta dawa ya kuwasaidia walemavu, watu wanaoishi katika mazingira magumu,
nasisi kama Waislamu wa Tanzania na waisokuwa waislamu wa Tanzania tutakapo
leta mshikamano huo, basi ninauhakika haya yote tutaweza kuyafanya na itakuwa
ile funga anayokusudia Mungu (swt) imefikia malengo.
Jambo la
pili funga inasababisha kuleta kuvumiliana, mungu anaposema kwamba ameleta
funga ili muwe wachamungu, moja ya sifa ya wachamungu wanatabia ya kuvumiliana,
kwa hivyo watanzania wanaombwa na kitabu cha mwenyezimungu (Qur’an) ambacho
kimeshuka katika mwezi wa ramadhani kwamba funga ifikie mahala watu
wanavumiliana.
Tofauti zao
za Madhehebu, tofauti zao za dini, tofauti zao za mitazamo, zinawafanya
hawawezi kubaguana, hawawezi kugombana, hawawezi kupigana, wala hawawezi kusutana,
hii ni sifa ya watu waliofunga na matarajio ya funga ya athiri kwa namna hiyo.
Jambo la
tatu mungu anaposema ametufaradhishia kufunga ili tuwe wachamungu, moja ya
maana ya uchamungu, ni watu kuwa kitu kimoja, na umoja hapa napenda
niuzungumzie umoja wa aina mbili:
Kwanza Umoja
wa Waislamu wenyewe kwa wenyewe, kamataneni na kama ya mwenyezimugu yote kwa pamoja
wala msifarikiane, nyote muwe kitu kimoja kuwakitu kimoja ni dalili ya
uchamungu.
Kuwa kitu
kimoja ni dalili ya kuwa mnamuabudu mungu wenu mmoja, kwahivyo ili funga yetu ikubaliwe, na ili funga yetu
ilete athari katika jamii, lazima waislamu ni watu wanaokusanywa na mwamvuli mmoja
Lailah ilallah, Muhammad Rasulullah, wafanye kila bidii kuhakikisha kwamba
wamekuwa kitu kimoja na siki zote umoja ni sababu ya nguvu katika jamii.
Pili ni
Umoja wa kati ya Watanzania pasina kujali na kujali dini zao, pasina kujali
madhehebu zao, mwenyezimungu anapotutaka tuwe wachamungu moja ya sifa ya
wachamungu ni watu wanopenda kuwa kitu kimoja.
Watanzania
waliofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na wale ambao hawakufunga wanaitwa wawe
kitu kimoja wungane , washikamane, umoja
tuliokuwa nao ambao hatujuani kwa makabila yetu, hatujuani kwa madhehebu zetu,
hatujuani kwa dini zetu,bali tunajuana kwa anuani ya utanzania.
Mwisho
naitakia Tanzania yenye kheri na Baraka na fanaka , naitakia Tanzania izidi
kuwa kisiwa cha amani na maelewano na pale ambapo panakosa amani basi
mwenyezimungu aparudishe pawe na amani kwa haraka iwezekanavyo, nawatakia Eid
njema, yenye Baraka yenye kheri, yenye mafanikio na Eid ipite kwa salama
salmini na zile sifa nzuri tuliokuwa nazo kipindi cha swaum ya ramadhani
ziendelee kuwepo katika jamii ya watanzania ili ziweze kuwaathiri watu wote na
nje ya mipaka yetu, namshukuru mungu .Asanteni sana.
Imetolewa na: