Friday, June 24, 2016

Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) chaadhimisha siku ya wajane Duniani

Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) chini ya Mwenyekiti Dada Rosse leo umeadhimisha Siku ya Wajane Duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar  ambapo hapa nchini ni maadhimisho ya mara ya pili.

Kwa mujibu wa TAWIA  wajane ni wengi sana zaidi ya wagane ambapo taasisi yao ina jumla ya wajane 700 na wagane 20 na imejipanga kuanzisha kituo cha pamoja ambacho kitasaidia wajane kupata  huduma za ushauri nasaha, msaada wa kisheria, uchumi na matibabu ili kupunguza kero wanazokutana nazo pindi wanapofiwa na wenza wao.

Aidha TAWIA imekemea vikali tabia ya wajane kunyanyaswa, pindi wanapofiwa na wenza wao kama kuitwa wachawi na kuhusishwa na vifo vya waume zao, kunyang’anywa mali, watoto na wengine kufukuzwa kwenye nyumba walizojenga na waume  zao wakati wa uhai wao.

Hata hivyo Mkurugenzi wa TAWIA, Rose Sarwat ameiomba serikali na taasisi zingine kuwaunga mkono katika harakati hizo.
Zifuatazo ni picha za maadhimisho hayo;













"Binaadam ni kiumbe Mtukufu,Walemavu wa Ngozi ni Watanzania" Sheikh Jalala



Kiongozi Mkuu wa Waislamu dhehebu la shia Ithnasheria Tanazaia Sheikh Hemed Jalala amesema Walemavu wa Ngozi ni Binaadam kama binaadam wengine (Watanzania), kwani binadam ni kiumbe kitukufu mbele ya Mwenyezimungu.

"jamii ifahamu kuwa hakuna njia ya mkato ya kupata utajiri na kwamba wale wote ambao wanaamini katika kuua watu wenye ulemavu wa ngozi ili wanufaike wanapaswa kuacha tabia hiyo kwani ni kwenda kinyume na mufundisho ya dini zote duniani"...

 "Wito kwa Watanzania kupinga mauaji ya Albino kwa vitendo na kuwataka viongozi wa dini kutumia membari zao kukemea viitendo viovu vya mauaji ya albino"amesisitiza Sheikh Jalala

Akizungumza katika iftari maalum na watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka Wilaya ya Kinondoni, hapa Masjid Ghadir, Kigogo-Post Dar es salaam, Sheikh Jalala amesema viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kulizungumza hilo bila woga kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi.
 
Amesema Albino ni binadamu kama walivyo watu wengine hapa nchini, wanahaki sawa ya kuishi, kulindwa na nyinginezo hivyo si haki kukatiza maisha ya watu hao na kwamba dini zote za duniani haziruhusu watu kuuana.

Aidha sheikh Jalala amefafanua njia nzuri za kupata utajiri kuwa ni kufanya kazi kwa bidii zote na si kuwaza Imaani potofu ya kuua watu wengine ambao hawana hatia.

Amesema kitendo cha kuua kinazima ndoto zao, hivyo ni wakati watu wakafahamu hilo na kuachana na tabia hiyo ambayo inatia doa Taifa la Tanzania huko Ulimwenguni.

“Nataka niseme, tendo la kuwaita wenzetu wenye ulemavu wa ngozi na kushiriki pamoja futari ya jioni hii ni kuonyesha kuwa hawa ni wenzetu, hawana utofauti wowote na wengine, wanahaki sawa kama Watanzania…kuwaua ni matendo ya kishetani na hayakubariki” alisema Sheikh Jalala.
 
Amesema wale wote ambao bado wana Imaani ya kuua ili watajirike ni washamba na hawajui walifanyalo, wanapaswa kufahamu kuwa utajiri hauletwi kwa damu za watu badala yake ni kujituma kwa kufanya kazi inayompendeza Mungu.

Katika hatua nyingine Sheikh Jalala amewaahidi chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi Wilaya ya Kinondoni kuwapa ushirikiano wowote watakaouhitaji na kwamba wanakaribishwa katika msikiti wa Kigogo  muda wowote na watapewa ushirikiano unaostahili.

“Nataka niwaambie ndugu zangu wenye ulemavu wa ngozi hapa Tanzania sisi hapa Kigogo tunawapenda na tunawakaribisha hapa msikitini ,sisi hatujui kubaguana,muone kama mko nyumbani na kwamba muda wowote mkiwa na haja ya kutuona milango iko wazi na mnakaribishwa sana ”Alisema Sheikh Jalala.

Akizungumzia Msikiti wa Kigogo Sheikh Jalala amesema ni kimbilio la watu wote, ni msikiti wa wakristo, watu wenye ulemavu wa ngozi, wajane na masikini. Ni msikiti ambao unajari imaani za watu tofauti kwani wanaamini kuwa haitokea siku moja nchi yote ya Tanzania kukawa na dini moja hivyo si wakati wa kubaguwana.

Haitakaa itokee Tanzania kukawa na dini moja mpaka dunia inapogota mwisho wake…lakini mtakubaliana na mimi kuwa Mungu aliyeumba Mkiristu ndiyo huyo aliyemuumba muislamu na wale wa Dini nyingine, Mwanzo wa binadamu ni uleule wa Adamu na hawa…tofauti zilizopo ni za kibinadamu hatuna haja ya kubaguana.Alisema.