Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) chini ya Mwenyekiti Dada Rosse leo umeadhimisha Siku ya Wajane
Duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo hapa nchini ni
maadhimisho ya mara ya pili.
Kwa mujibu wa TAWIA wajane ni wengi sana zaidi ya wagane ambapo
taasisi yao ina jumla ya wajane 700 na wagane 20 na imejipanga kuanzisha
kituo cha pamoja ambacho kitasaidia wajane kupata huduma za ushauri
nasaha, msaada wa kisheria, uchumi na matibabu ili kupunguza kero
wanazokutana nazo pindi wanapofiwa na wenza wao.
Aidha TAWIA imekemea vikali tabia ya wajane kunyanyaswa, pindi
wanapofiwa na wenza wao kama kuitwa wachawi na kuhusishwa na vifo vya
waume zao, kunyang’anywa mali, watoto na wengine kufukuzwa kwenye nyumba
walizojenga na waume zao wakati wa uhai wao.
Hata hivyo Mkurugenzi wa TAWIA, Rose Sarwat ameiomba serikali na taasisi zingine kuwaunga mkono katika harakati hizo.
Zifuatazo ni picha za maadhimisho hayo;
No comments:
Post a Comment