Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa Khutba ya Swala ya Ijumaa, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema
kuwa katika jambo la kusikitisha na kuhuzunisha leo katika Ulimwengu wa
Kiislamu ni kundi la Kiwahabi kufanya bidii na mikakati ya hali na mali,
mikakati ambayo ni ya kuwagawa Waislamu, kuhakikisha Waislamu hawezekani wakawa
kitu kimoja.
Maulana Sheikh Jalala alisema hayo jana katika
Khutba ya Swala ya Ijumaa, iliyoswaliwa Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es
salaam,akizungumzia Je, Uwahabi na Usuni ni Kitu Kimoja?, na kusema kuwa Kundi
la Kiwahabi limefanikwa kuingia katika Jamii ya Waislamu Ahlul Sunna na kujiita
wao ni Ahlul Sunna.
Maulana Sheikh Jalala alisema kuwa Mafundisho ya Mtume Muhammad
(s.a.w.w) na Swalafun Swaleh yanaharamisha Kumkufurisha Mtu anaetoa Shahada
Mbili hatakama mnatofautiana rai, lakini jambo la kushangaza kundi la Kiwahabi
wanakufurisha Mtu anaetoa Shahada Mbili kwa kuwa wanatofautiananae rai.
“Watu walikuwa wamoja, Waislamu walikuwa ni Kitu kimoja,
kutoka Mtume Muhammad (s.a.w.w), Moja ya jambo ambalo ukilisoma katika historia
ya kipindi hicho cha watu ambao ni Salafun Swaleh, moja ya kitu walichokuwa
wanapambana nacho na hawakikubali ni jambo la kumkufurisha mtu anaetamka
Shahada Mbili, ila Kundi la Kiwahabi linakufurishana” alisema Maulana Sheikh
Jalala.
Maulana Sheikh Hemed Jalala aliongeza kuwa kundi la Kiwahabi
ndio kundi cha kwanza kuzuka duniani lililokuja kumkufurisha mtu wa Qibla, na
kuhalalisha Umwagaji wa Damu yake na Unyaganyi wa Mali zake na kusema kuwa hayo
sio Mafundisho ya Ahlul Sunna.
“Kundi la Kiwahabi lilipokuja,
lilipodhihiri, lilipozuka Duniani ndio Kikundi cha kwanza lililokuja
kumkufurisha Mtu wa Qibla, yani Mtu anaesema Ashahadu allaa illaah ilallah
waashahadu anna Muhammad Rasulullah, kwa kuwa hakubaliani na fikra zao huyo ni
Kafiri, na damu yake ni halali na mali yake ni hali” aliongeza Maulana Sheikh
Jalala.
Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala alisisitiza kuwa Jamii ya
Kiislamu haina misamiati ya kukufurishana wala kuitana Mushriki kwa watu
wanaotoa Shahada Mbili, kwasababu wanatofautiana rai na mtazamo na kusema kuwa
hayo sio Mafundisho ya Ahlul Sunna.
“Jamii ya Waislamu haijazoea, haijasikia wala haijalelewa
katika Misamiati hii huyu ni kafiri, huyu ni Mshirikina, haipo kwenye kamusi ya
Kiislamu, kwa waislamu wenyewe kwa wenyewe kutuhumiana na Shirki, kwa kosa
gani? Kwa kosa la kutoafautiana rai na mtazamo ambapo sio Mafunzo na Maelekezo
ya Maimam wanne wa Ahlul Sunna”alisisitiza Maulana Jalala.