Saturday, May 2, 2015

Nafasi ya Dini katika kutangaza na kueneza Haki za Wanawake na Uadilifuk kwa jamii

Dkt. Riziki Ngwela, akitoa mada ya "Ushirikiano wa Madhehebu za Dini mbalimbali katika kuleta jamii ya Wanawake na KuzuiaUnyanyasaji dhidi ya Wanawake na Watoto.          Amesama kuwa Taasisi za Kidini zinapaswa kuhubiri maneno ya Mungu, kuelimisha na kusisitiza juu ya Ushirikiano na kutambuana. Aidha amesema kuwa zinapaswa kujenga Uadilifu katika jamii, ili kuleta amani na uongofu.
Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba yake katika semina iliyokusanya dini kuu mbili ya Uislamu na Ukristo katika kujadili "Nafasi ya Dini katika kutangaza na kueneza Haki za Wanawake na Uadilifu wa jamii", iliyoandaliwa na Ofisi ya Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Kiislamu wa Iran.       Sheikh Jalala amesema kuwa Imam ali (a.s) alisema Mwanadamu ametunukiwa Vitu muhimu Viwili, kati ya hivyo ni Amani, hiyo amewataka Watanzania kuienzi amani .Aidhaa amesema kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), kama ni siku ya Amani, Upando , Ushirikiano, kuvumiliana.

Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA), Mama Shamim Khan, akitoa muongozo juu ya Watoa Mada, Pembeni yake ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, hapa Tanzania.

Mchungaji Rev, Thomas Father Goda akitoa mada yake inayosema "Nafasi ya Dini katika Kujanga na Kueneza Amani na Uadilifu wa Jamii kwa Wanawake"

Katikati ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam wa Iran, akitoa shukrani na pembeni yake kulia ni Muakilishi wa Utamaduni wa Iran hapa Tanzania.

Kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s) ni siku ya Kusameheana

Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba leo mbele za waumini wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la Shia, katika Warsha ya Kukumbuka ya kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s) iliyoandaliwa na Uongozi wa Chuo cha Kidini cha Jamia Mustwafa, Upanga, Dar es salaam. 

Na amesema kuwa Imam Ali (a.s) alikuwa ni mtu wa watu wote na kwa mambo yote.Aidha amesisitiza kuwa siku ya Kuzaliwa Imam Ali(a.s) ni siku ya kusameheana,kusahau matatizo yetu,tofauti zetu na ni siku ya Umoja.

Imam Ali (a.s) alizaliwa tarehe 13 Rajabu Mwaka 600AD.Wazazi wa Imam Ali(a.s) ni Baba Abu Twalib bin Abdul mutwalib na Mama Fatma bint Asad.

Viongozi, Wanatabligh pamoja na Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza hotuba aanayoitoa Maulana Sheikh Hemed Jalala.
 Sheikh Ghawth Nyambwa ni mmoja wapo katika Viongozi wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s), akitoa hotuba na Kusema kuwa Imam Ali (a.s) aliweza kuishi na kila mtu bila kujali dini wala tofauti walizokuwa nazo.

Aidha amewataka wafuasi wa Ahlulbayt (a.s) kufikiria jukumu la kueneza Mafundisho sahihi ya Dini ya Kiislamu ni jukumu la kila mtu,bali siokufikiria jukumu hilo ni la mtu fulani

Maulana Hemed Jalala 'aungana katika kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w)'


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisalimiana na Viongozi wa Hawzat Imam Swadiq (a.) katika Sherehe za Kumbukumbu za Mtume Muhammad (s.a.w.w).


Kumbukumbu hizo zimefanyika leo usiku katika viwanja vya Kigogo Roud About, jijini Dar es salaam, iliyoandaliwa na Waislam wa Dhehebu la Sunni.


Mwalim Mkuu wa Chuo cha Kiislam cha Misri hapa Dar es salaam, Tanzania akitoa hotuba ilisotoa sifa kwa Mkoa wa Dar es salaam,kuwa ni Mkoa wenye kumpenda sana Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba yake iliyoaanza kwa kuuliza "Madrasa ni nini" mbele ya Waumini wa Dini ya Kiislam.
 “Taifa hili kama lina hitajia kuifunga Taasisi ya Takukuru, kupata wakusanyaji kodi wazuri, rai wema na wasio waovu, na wala Rushwa basi ni kuzienzi madrasa, na akaitaka wizara ya elimu kuzienzi madrasa hizo na kuzitia nguvu kwa kuzipa posho kwani kazi zinazofanya zina mchango mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla." Amesema Sheikh Jalala.
 Aidha Maulana Hemed Jalala ametoa wito kwa Taifa la Tanzania kama linahitaji watumishi wenye maadili mema ni lazima kuzienzi Madrasa.
Hawa ni baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiume wakiwa makini katika kusikiliza Sifa na Mashairi mbalimbali za Kumsifu Mtume Muhaammad (s.a.w.w)