Saturday, May 2, 2015

Kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s) ni siku ya Kusameheana

Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba leo mbele za waumini wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la Shia, katika Warsha ya Kukumbuka ya kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s) iliyoandaliwa na Uongozi wa Chuo cha Kidini cha Jamia Mustwafa, Upanga, Dar es salaam. 

Na amesema kuwa Imam Ali (a.s) alikuwa ni mtu wa watu wote na kwa mambo yote.Aidha amesisitiza kuwa siku ya Kuzaliwa Imam Ali(a.s) ni siku ya kusameheana,kusahau matatizo yetu,tofauti zetu na ni siku ya Umoja.

Imam Ali (a.s) alizaliwa tarehe 13 Rajabu Mwaka 600AD.Wazazi wa Imam Ali(a.s) ni Baba Abu Twalib bin Abdul mutwalib na Mama Fatma bint Asad.

Viongozi, Wanatabligh pamoja na Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza hotuba aanayoitoa Maulana Sheikh Hemed Jalala.
 Sheikh Ghawth Nyambwa ni mmoja wapo katika Viongozi wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s), akitoa hotuba na Kusema kuwa Imam Ali (a.s) aliweza kuishi na kila mtu bila kujali dini wala tofauti walizokuwa nazo.

Aidha amewataka wafuasi wa Ahlulbayt (a.s) kufikiria jukumu la kueneza Mafundisho sahihi ya Dini ya Kiislamu ni jukumu la kila mtu,bali siokufikiria jukumu hilo ni la mtu fulani

No comments: