Sunday, January 24, 2016

Sheikh Jalala "Vyombo vya Ulizi na Serikali, Uislam hauna Mahusiano na Ugaidi"

Mmoja wa Viongozi wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala amevitaka Vyombo vya ulinzi nchini pamoja na serikali kwa ujumla kutambua pamojana kuelewa kuwa vitendo vya ugaidi vinavyotokea nchini Poamoja na duniani kwa ujumla havina uhusiano wowote na dini ya kiislam kama jinsi ilivyokaririwa na wengi.
 
“Makundi mbalimbali kama Al shabab, Bokoharam, Daesh na mengineyo yote yanayojinasibisha na Uislam, ambao utawakuta wanabeba bendera imeyoandikwa Laillaha Illa llah, Muhammad Rasulullah, hao sio waislam,kwaniUislam hauruhusu kumwaga Damu ya Mtu.”amesema Sheikh Jalala


Sheikh Jalala amesema kuwa moja ya sababu ya Ugaidi ni kuwa na fikra ya Kukufurishana,ambapo inafikia watu wanaitana majina mabaya,na kukufurishana inamaanakuwa damu yake ni halali,ambapo ni kinyume na mafundisho ya Uislam ambao aliokujanao Mtume Muhammad (s.a.w.w).


“Dini ya Kiislam sio dini inayolingania mauaji bali ni dini inayolingania amani, maelewano,kuvumiliana, kuelewana, kuoneana huruma na mshikamano bila kujali itikadi za kidini, kikabila, kitaifa na wala kirangi, bali Uislam unalingania amani kwa watu wote” amesisitiza Sheikh Jalala.


Haya ameyasema leo katika Semina  inayozungumzia Changamoto zinazowakabili Ummah wa Kiislam nchini na Duniani kwa Ujumla katika Lamada Hotel, ambayo iliyoandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhar Foundation,chini ya Sheikh Khalifa Khamisi.


Aidha Sheikh amesema kuwa nchi ya Tanzania ni moja kati ya nchi chache duniani ambazo zinaishi kwa umoja na mshikamano pamoja na upendo wa hali ya juu hivyo semina hiyo itatumika kuwatahadharisha watanzania kuepuka sana kukaribisha vitendo vya kigaidi katika nchi yao kwani itasababisha hatari kubwa.


“Kuwa semina hiyo imekuja mahususi kuwakumbusha waislam jukumu lao la kujenga umoja miongozi mwao na kwa watanzania kwa ujumla jambo ambalo litasaidia katika kuendeleza umoja na mshikamano wa watanzania uliopo”.ameongeza Sheikh Jalala.

Hatahivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhar Foundation Sheikh Khalifa Khamisi amesema kuwa leo akipatikana mtu mmoja ambaye kavaa kanzu kafanya vitendo vya kigaidi basi inachukuliwa kuwa waislam woote ni magaidi dunian,sio kweli na hatufundishi ugaidi katika dini zetu,tunaomba vyombo vya dola kufuta mawazo haya mabaya juu ya uislam”amesema.


“Kwa sasa waislam wamekuwa Wahanga kwa kutuhumiwa kuwa wao ndio Magaidi kwa kuwa wanafanya mambo ya kumkera mwenyezi mungu kwa kuwafanyia wenzao mambo ya maovu jambo  aliendani na mafundisho ya Dini ya Uislam ambapo jambo hili sio kweli bali ni fikra pandikizi zilizopandwa na maadui wa Uislam”amesema Sheikh Khamisi.


Sheikh Khamis amesema kuwa dini ya kiislam haina mahala popote inapofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi,mauaji,na vitendo vya kinyama vinavyotendeka duniani hivyo ni lazima watanzania na dunia kwa ujumla kuacha kuamini kuwa vitendo vya kigaidi vinafanywa na waislam.