SERIKALI imejigamba itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kupeleka nishati ya
umeme vijijini. Charles Mwaijage, naibu
waziri wa nishati na madini, ameliambia bunge mjini Dodoma, kuwa serikali
inaendelea kukarabati njia za umeme katika wilaya zote nchini. Anaandika
Dany Tibason … (endelea).
Mwijage alikuwa
akijibu swali lililoulizwa na mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR- Mageuzi), Moses
Machali.
Katika swali lake la msingi,
Machali alitaka kujua kama
serikali haioni umuhimu kukarabati nyaya, mita na
vifaa vingine ili kuhakikisha umeme takribani megawati 2 hazipotei kama ilivyo
sasa.
Machali alitaka kufahamu
utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyotoa bungeni katika mkutano wa bajeti wa
mwaka 2013 ambako iliahidi kusambaza umeme katika vijiji vya Nyumbigwa,
Murufiti, Kidyama, Herujuu Mganza, Ruhita na Kanazi.
Mwijage amesema vifaa vya
kujenga miundombinu ya umeme vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi na vinaendelea
kupelekwa Kasulu ambapo wateja wanaendelea kuunganishiwa umeme.
Amesema umeme
unaozalishwa haupotei kama ilivyokuwa hapo awali baada ya wateja 4,400
kuunganishiwa umeme hivyo kufanya wateja 4,700 kunufaika na huduma ya umeme kwa
sasa kutoka wateja 300 mwaka 2011.