Friday, January 8, 2016

PROF. MBARAWA: SERIKALI HAITAWAVUMILIA WATUMISHI WAZEMBE

MB1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Mwenge – Moroco KM 4, kuhakikisha inajengwa kwa ubora uliokusudiwa na kukamilika kwa wakati ili kumaliza adha ya msongamano wa magari katika eneo hilo.

Akikagua ujenzi wa barabara hiyo Prof. Mbarawa amemtaka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na hatua kali zinachukuliwa kwa watu wote watakaozembea na kuhujumu miradi ya barabara.
“Kipaumbele chenu kiwe ubora na kufanya kazi kwa haraka ili barabara hii ikamilike katika wakati uliopangwa na hivyo kuondoa usumbufu kwa wananchi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Akizungumza na wafanyakazi wa TANROADS makao makuu Prof. Mbarawa amesema serikali haitawavumilia watumishi wazembe wanaofanya kazi chini ya kiwango au kwa uzembe.
Amewataka TANROADS kuhakikisha hakuna misururu mirefu katika vituo vya mizani zote nchini na kupambana na rushwa katika ngazi zote ili kulinda fedha za serikali na kukuza uchumi.
 MB2
Akizungumza na watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa kutopeleka fedha za mfuko wa barabara kwa halmashauri zinazoshindwa kujenga barabara bora na kuzitaka halmashauri zote kuhakikisha fedha zinazopelekwa zinawiana na  miradi inayojengwa.

“Bila miundombinu ya kisasa hatuwezi kujenga uchumi tutumie fursa tuliopewa kuwatumikia watanzania kwa moyo wa uzalendo ili kukuza uchumi wa nchi”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Bw Joseph Haule amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa bodi hiyo inayohudumia barabara zenye urefu wa KM zaidi ya elfu 252 katika halmashauri 166 nchini imejidhatiti kuhakikisha fedha za mfuko wa barabara zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa  ili kuimarisha sekta ya uchukuzi na kukuza uchumi.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa ametembelea Bodi ya Wahandisi (ERB), Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) na Bodi ya Makandarasi (CRB) na kuagiza kurahisisha mchakato wa usajili ili kuvutia wataalam wengi wa fani za ujenzi kujisajili katika bodi hizo na kupunguza watendaji wasio na sifa.

“Sekta ya miundombinu ndio chanzo cha mafanikio ya nchi yoyote duniani hivyo fanyeni kazi kwa weledi na kuzingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili nchi ipige hatu za haraka kimaendeleo”.
MB3
Naye katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano sehemu ya ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amezungumzia umuhimu wa bodi hizo kujitangaza katika vyuo vikuu ili kuvutia wanafunzi wengi kusoma fani za kihandisi na kuongeza idadi ya wahandisi hapa nchini.

Amezitaka wakala na bodi zinazohusika na ujenzi kuongeza ubunifu ili kutoa huduma bora na kuiwezesha serikali kufikia malengo yake kwa wakati.

Waziri Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi na kutoa mwongozo wa namna ya kuitekeleza kwa wakati ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO

SERIKALI YATOA PICHA RASMI YA RAIS

????????????????????????????????????Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa akionesha picha ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa matumizi ya maofisini.
Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog
………………………………………………………..
IDARA ya Habari Maelezo imetangaza rasmi upatikanaji wa picha ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa matumizi ya maofisini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Msaidizi wa idara hiyo, Zamaradi Kawawa, alisema kila nakala ya picha hiyo bila fremu itauzwa kwa Sh 15,000 pamoja na picha ya Baba wa Taifa itauzwa Sh 5000 katika ofisi hizo.
Alisema picha ya Rauis na ile ya Baba wa Taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Tasisi za umma, Mashirika na ofisi binafsi.
“Serikali inatoa onyo kwa wale wote waliokuwa wakitundika picha ya Rais isiyo rasmi, wanatakiwa wazitoe haraka na waje katika ofisi zetu wanunue picha rasmi,” alisema Kawawa.
Aidha alisema picha hizo zitauzwa katika ofisi za Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), ambazo zimesambaa nchi nzima, hivyo watu wa mikoani watazipata katika Ofisi hizo.
Alipoulizwa kuhusu picha hiyo kucheleweshwa Kawawa alisema ilichelewa kutokana na picha iliyotolewa mwanzo kutokuwa na bora na kuwalazimu kurudia kutengeneza nyingine ambayo kimsingi inaubora wa kuridhisha.

Wimbi la chuki dhidi ya Waislamu lashadidi Ufaransa

Wimbi la chuki dhidi ya Waislamu lashadidi UfaransaWimbi la chuki dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada limezidi kuongezeka nchini Ufaransa.

Gazeti la Ufaransa la Le Figaro limeinukuu polisi ya mji wa Perpignan, kusini mwa nchi hiyo ikitangaza kuwa, vitendo vya chuki vinavyoambatana na vitisho dhidi ya jamii ya Waiislamu vinaonekana kuongezeka zaidi Ufaransa.

Kwa mujibu wa polisi ya mji huo, hivi karibuni kumezuka watu ambao wamekuwa wakichora picha na maneno ya kukashifu dini ya Kiislamu na wafuasi wa dini hiyo tukufu kwenye kuta za misikiti na hivyo kuwaweka Waislamu katika hali ya wasi wasi.

Gazeti la Le Figaro limemnukuu Yannick Janas, kamanda wa polisi wa eneo la Perpignan la kusini mwa Ufaransa, akisema kuwa, hivi karibuni watu wasiojulikana walichora picha ya mtu aliyekatwa kichwa na mikono kwenye kuta za msikiti mkuu wa mji huo na kwamba hivi sasa polisi wameanzisha uchunguzi wa kuwabaini wahusika wa picha hizo.

Hujuma na chuki dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa ziiliibuka baada ya mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 7 Januari na tarehe 13 Novemba mwaka jana wa 2015.chanzo irib

Maelfu waandamana kuulani jinai za Aal Saud duniani

Maelfu waandamana kuulani jinai za Aal Saud dunianiMaelfu ya Waislamu katika nchi mbalimbali za duniani wamefanya maandamano makubwa ya kuulani jinai za utawala wa Saudi Arabia kufuatia utawala huo kumuua shahidi Shaikh Nimr Baqir al-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kishia nchini humo.
Leo Waislamu nchini Iran walimiminika mabarabarani katika miji yote baada ya sala ya Ijumaa na kulaani jinai za Aal Saud katika eneo hili.

Waandamanaji hao sambamba na kusema kwa saudi kubwa: "Kifo kwa Marekani, kifo kwa Israel na kifo kwa Aal Saud," wamelaani vikali hatua zilizo dhidi ya binaadamu zinazofanywa na watawala wa Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati hususan nchini Yemen, Syria na Iraq na kuutaja utawala huo kuwa ni kiini cha matatizo ya Waislamu duniani.

Mbali na Iran, maandamano makubwa kama hayo yamefanyika katika nchi mbalimbali ikiwemo Pakistan ambapo waandamanaji wamewalaani watawala wa Aal Saud, na kubeba mabango na picha za shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Aidha waandamanaji wamemtaja shahidi Sheikh Nimr kuwa mfano wa kuigwa na mwanamapambano mkubwa ambaye licha ya mashinikizo mbalimbali kutoka kwa utawala wa Saudia, hakurudi nyuma katika azma yake ya kutetea haki za raia wa nchi hiyo.

Wapakistan pia wameitaka serikali ya Islamabad kukata mara moja uhusiano wake na Saudia ambayo wameitaja kuwa ni nchi yenye utawala unaolea magaidi na kuwakandamiza Waislamu.chanzo irib

SALAAM ZA PONGEZA KWA MAZAZI YA NABII ISSA AS, (YESU) KWA WAKRISTO WOTE.



Akitoa  salaam   za Krismas  na  Mwaka  Mpya kwa  wakristo wote  Duniani,,  katika  mkutano  na waandishi  wahabari  uliofanyika leo katika  Hawzat Imam Swadiq  Dar es slaam, Sheikh Hemed  Jalala amesema: sisi  kama waislaam, viongozi  wa dini, watanzania, kama wanaadam , tunayohaki  ya kuwapa mkono wa  kheri  ya  krismas   kwa kusema tupo pamoja  katika  kusheherekea mazazi  ya Issa  as, au  Yesu .
 
Sheikh Jalala amesema: sababu kubwa  iliyotufanya  kuwaita  vyombo  vya  habari  ni  kuwatangazia  kua: wakristo ni ndugu zetu, ndugu zetu katika  asili moja, sote  tunatokana na Baba mmoja  Adam (a.s) na Hawaa ( Eva).” Wakristo  na  waislaam  wote  baba yao  ni Adam na  mama  yao ni Hawa, kwanini  tusipongezane  wakati sisi  ni waasili  moja?  Tofauti  tulizo nazo  hazivunji  udugu huu  wa kiasili:   Mwenyezi  Mungu  (S.W)  amesema  katika  surat Hujurat : 

39-13  Enyi watu  hakika  ni mekuumbeni  kutokana na  mwana mke  mooja  na mwanamume  mmoja, natukawafanya  mataifa  na  makabila  ili mjuane, hakika  mbora wenu  ni mchaji  mungu sana. Sisi  ni ndugu  kwa kua  ni watu  wa  Imani,  sote tunaamini  mungu  mmoja japo kua kuna  tofauti ndogondogo, tunaamini  kua  ipo siku ya  mwisho , siku  ya  kuhesabiwa.

Tunaamin  vitabu  4: Vilivyoletwa  kwa mitume  kuja kuwaongoza watu.  Taurati aliyopewa  Nabii  Musa  (a.s)  Zabuur  aliyopewa  Nabii Daud (a.s), Injili  aliyopewa  Nabii Issa (a.s), (Yesu). Na  Qur aan  aliyopewa Mtume Muhammad  (s.a.w.w), ikiwa  wakristo  wanaamini  katika  Tourat, injili  na  Zabuur,  ni mahala  pake  kuwapongeza, kwa  ni watu  wa  kitabu, hata Qur aan  inawaita  kwa  majina  mazuri  , Enyi  watu  wa kitabu. 

Waislaam  wanawaangalia   wakristo kua ni  ndugu  zetu, wanzetu, wanaadam wenzetu na wala  si   maadui,  ndio  maana mtume  Muhammad  (s.a.w.w) aliishi nao  vizuri  makkat  na  madina ,na kuwekeana  nao  Makubaliano  ya  kuishi  kwa  Amani.”  kwahiyo  tunayo hakki  ya  kuwaambia  ndugu  zetu   wakristo  kua  tupo  pamoja  katika  sikukuu  hii  ya  kuzaliwa  kwa  Nabii  Issa  as,  (Yesu).  

Na kwa  kua  sisi kama  Watanzania  na  wadau  wa Amani ,Tunaamini  vikao  kama hivi   vinajenga  na  kuimarisha  umoja  huu  na  mshikamano kwa  viongozi  wa  dini  na  waumini  kwa ujumla,mungu  Ibariki  Tanzania, Mungu  Ibariki Afrika,, na  viongozi  mungu  awatie  nguvu na  afya  njema  katika  kuwahudumia  wananchi  wao, Ahsanteni  sana.

Katika Quran Mungu anasema “Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi” surat Maida aya 82.

Ewe Nabii! Tunakuhakikishia ya kwamba utaona hapana watu wanao kuchukia na kukubughudhi wewe na wanao kuamini kama Mayahudi na hawa wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Na utawakuta walio karibu mno nawe kwa mapenzi ni wafwasi wa Isa, walio jiita wenyewe "Manasara". Kwa sababu wamo miongoni mwao makasisi wanao ijua dini yao, na marahibu (mamonaki) wat'awa, wanao mcha Mola Mlezi, na kuwa wao hawana kiburi cha kuwazuia wasisikie Haki. 

(Na haya yameonakana kuwa Waislamu wengi duniani asili yao walikuwa Manasara, Wakristo. Wao wakisha pata fursa ya kuufahamu Uislamu huufuata, lakini ni wachache miongoni mwa Mayahudi walio silimu. Kinacho wazuia ni kiburi. Lakini walio silimu basi wamekuwa Waislamu wakubwa.)
Na Imam Ali (a.s) anasema Udugu udupo wa aina mbili moja ni Udugu wa kuwa nyinyi ni Dini moja yaani nyinyi nyote ni Waislam pili Nyinyi mnatkana na asili moja yaani sote ni binaadam baba yetu ni Nabii Adam na Mama yetu ni Hawa (Eva).
Mwisho katika kuonyesha umoja wetu tumeandaa kadi za pongezi rasmi kupitia Ofisi yangu zikiambatana na zawadi ndogo kwa baadhi ya makanisa ili wapokee kwa niaba ya waumini wao, tunawaomba wazichulie zawadi zetu ndogo kama ishara ya upendo, umoja, maelewano na amani baina yetu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Sheikh Hemed Jalala,
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania. Pia ni Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam cha Imam Swadiq