Walimu wa Hawzat Imamu Jafari Swadiq (a.s) wakiwa katika
majlisi ya kukumbuka kifo cha Imam Mussa al-Kadhim.
Imam Kadhim AS alisisitiza kuhusu ufahamu na uono wa
mbali katika dini kwa kusema: ‘Ifahamu dini, kwani kuifahamu dini ni ufunguo wa
uono wa mbali na ubora wa ibada na ni njia ya kufika kwenye nafasi ya juu na
adhimu katika dini na dunia.
Ubora wa kufahamu dini ikilinganishwa na kufahamu
ibada ni sawa na namna jua lilivyo katika nafasi ya juu kuliko nyota. Kila
ambaye hafuatilii suala la kuifahamu dini, Mwenyezi Mungu hafurahii ibada yake.
|