Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro amesema katibu mkuu
wa chama hicho, Maalim Seif hana sababu ya kujibembeleza kwa Rais wa
Zanzibar, Dk Mohamed Shein kwa sababu masuala ya maslahi kwa viongozi
wastaafu ni ya kikatiba na kisheria na hayatolewi kwa hisani ya mtu.
Akizungumza
leo kufuatia kauli ya Rais John Magufuli jana akiwa ziarani visiwani
humo kwamba Dk Shein asingesaini posho na matibabu kwa ajili ya Maalim
Seif kwa vile alikataa kusalimiana naye, Mtatiro alisema viongozi
wastaafu wanastahili kupata matibabu na posho nyingine kwa mujibu wa
Katiba na sheria za nchi.
“Tunataka kumweleza Rais Magufuli kwamba
Dk Shein hana uwezo wa kufuta matibabu na posho kwa Maalim Seif kwa
kuwa yapo kikatiba na kisheria,”alisema.chanzo.mwananchi
Kigoma. Kukua na kustawi
kwa vyama vya siasa kuanzia mfumo huo ulipoanzishwa mwaka 1992 hadi
sasa, kumetokana na huruma ya marais waliotangulia kabla ya awamu
iliyopo sasa.
Kauli hiyo ilitolewa na mtaalamu wa elimu na
saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitilla
Mkumbo alipozungumza na baadhi ya wakazi wa Mji wa Kigoma kupitia asasi
ya Meza ya Duara ya Watanganyika iliyopo Soko la Mwanga mjini hapa.
Hata
hivyo, Profesa Mkumbo alisema anapongeza kitendo cha Rais John Magufuli
kuzuia maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, kwa vile jambo
hilo litawazindua Watanzania kudai Katiba bora ya nchi itakayojenga
misingi ya uwajibikaji kwa kila mmoja na kuheshimu sheria.
“Lazima
tumpongeze Rais wetu kwa kuzuia mikutano, maandamano na ubabe wa baadhi
ya vyama vya siasa, anasaidia sana kukomaza vyama. Kukua kwa vyama vya
siasa kulitokana na roho nzuri za marais waliotangulia, lakini sheria za
nchi hii ni mbovu,” alisema.chanzo.mwananchi
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewatuhumu majaji
wa mahakama za nchi hiyo kuwa wazembe kwa kuruhusu maandamano ya kupinga
serikali ambayo baadaye yaligeuka kuwa ya fujo na machafuko.
Mugabe alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa tawi la
vijana la chama tawala cha ZANU-PF, siku mbili kabla ya Mahakama Kuu
kusikiliza shauri la kupinga uamuzi uliotolewa wiki iliyopita wa kupiga
marufuku rasmi maandamano ya upinzani.
Serikali ya Zimbabwe ilichukua uamuzi wa kupiga marufuku kwa muda wa
wiki mbili maandamano yote katika mji mkuu Harare ambao umekuwa
ukishuhudia maandamano ya kulalamikia utendaji wa Rais Mugabe katika
kushughulikia matatizo ya uchumi, uhaba wa fedha na ukosefu wa ajira
nchini humo.
Kwa mujibu wa toleo la leo la gazeti la Sunday Mail, Rais Mugabe
aliuambia mkutano huo wa vijana wa chama chake tawala kuwa "hawezi
kuvumilia tena" na kwamba hatoruhusu maandamano ya fujo na machafuko
yaendelee kufanyika.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Mugabe amesema mahakama, mfumo wa sheria na
majaji wa Zimbabwe wanapaswa kuwa watu wenye uelewa zaidi kuliko raia
wa kawaida na kwamba wasizembee katika maamuzi wanayotoa wakati
yanapowasilishwa maombi na watu wanaotaka kuandamana.
Kufuatia kauli hiyo ya Rais Mugabe, kiongozi wa chama cha
Kidemokrasia cha Wananchi, Tendai Biti na ambaye pia
ni mwanasheria aliyeongoza mpango wa kuwasilisha shauri la kupinga
marufuku ya maandamano iliyotangazwa hivi karibuni, amemtuhumu Mugabe
kuwa anatoa vitisho dhidi ya mahakama na kukiuka katiba.
Wakiongozwa na Biti, wanaharakati kadhaa wa kisiasa wamewasilisha
shauri katika Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo wa serikali wakisema kuwa
ni kinyume na Katiba. Shauri hilo linatazamiwa kusikilizwa hapo kesho.
Askofu Nicholas Chamberlain wa Grantham nchini
Uingereza amekiri kuwa ni shoga, na kwamba Askofu Mkuu wa nchi hiyo
alijua suala hilo kabla ya kumteua kuwa askofu.
Askofu Nicholas Chamberlain amesema amekuwa shoga kwa muda
mrefu na kwamba amekuwa na mahusiano ya kingono na mwanaume mwenzake.
Chamberlain anakuwa askofu wa kwanza wa Kanisa la Uingereza (Church
of England) kukiri kwamba ni shoga na amelazimika kukiri baada ya gazeti
la Sunday kutishia kwamba, litafichua na kuanika wazi tabia hiyo.
Vyombo vya habari vinasema, suala hilo yumkini likazusha makelele mengi kati ya wafuasi wa kanisa hilo nchini Uingereza.
Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby amekubali kwamba alikuwa na
habari kwamba askofu Nicholas Chamberlain ni baladhuli na shoga na
kwamba alimteua kuwa askofu kutokana na umahii wake.
Gazeti al The Guardian la Uingereza limeandika kuwa, katika siku za
hivi karibu maaskofu wengi wa Uingereza wamefunga ndoa na mashoga
wenzao.
Bikizee mmoja wa miaka 87 amehukumiwa kifungo cha
miezi minane jela na mahakama moja ya nchini Ujerumaini kwa kosa la
kukanusha tukio lililojaa utata la kuuliwa kwa umati Mayahudi nchini
humo, maarufu kwa jina la ngano ya Holocaust.
Shirika la habari la Ujerumaini
limeripoti habari hiyo n akuongeza kuwa, Ursula Haverbeck, bikizee
mwenye umri wa miaka 87 raia wa Ujerumani kwa mara nyingine amekanusha
kutokea mauaji hayo na mahakama ya Detmold imeamua kumfunga jela miezi
minane.
Akielezea msimamo wake usiotetereka,
Bikizee huyo amesema, Mayahudi walikuwa wakiishi maisha salama na ya
kawaida katika kambi ya Wanazi ya Auschwitz, na kamwe hawakuwa
wakiadhibiwa bali hiyo ilikuwa ni kambi ya wafanyakazi wa kawaida tu.
Mahakama nyingine kadhaa zimewahi kutoa
hukumu dhidi ya bikizee huyo kutokana na kukanusha mauaji hayo
yanayodaiwa kufanywa na Wanazi wa Ujerumaini dhidi ya Mayahudi.
Wazayuni wanatumia vibaya madai ya
kutokea mauaji hayo ili kupokea fidia hadi leo hii, kama ambavyo
wameyafanya kisingizio cha kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Ujerumani nayo inajinadi duniani kuwa ni
dola lililopiga hatua kubwa za kidemokrasia na kwamba eti watu nchini
humo wana uhuru kamili wa kuelezea misimamo yao.
Hata hivyo kufungwa jela bibi huyo mtu
mzima kwa kosa la kutangaza msimamo wake kuhusu ngano ya Holocaust
kunatilia shaka mno madai ya kuweko demokrasia na uhuru wa kusema katika
nchi za Magharibi ikiwemo Ujerumani.
Ngano ya Holocaust ni mstari mwekundu
kwa nchi za Magharibi na hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya
uchunguzi kuhusiana na uhakika wa ngano hiyo kwani Holocaust ndiyo
falsafa ya kuanzishwa utawala wa Kizayuni wa Israel na manufaa muhimu
mno ya Uzayuni wa kimataifa wa madola ya Magharibi yamo ndani ya ngano
hiyo.
Ujumbe maalumu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
(ICC) unaelekea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa
madhumuni ya kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na utawala wa
Kizayuni katika vita vya siku 50 dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Duru za habari zimeripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel
unajiandaa kuupokea ujumbe huo ambao unatazamiwa kufanya uchunguzi
kuhusu tuhuma za jinai za kivita ambazo utawala huo haramu unatuhumiwa
kuzifanya wakati wa vita vya mwaka 2014 dhidi ya Wapalestina wa Gaza.
Safari ya ujumbe huo wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ambayo
itafanyika hivi karibuni imetokana na ombi la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa
mahakama hiyo Bi Fatou Bensouda na lengo lake ni kutoa fursa kwa
wajumbe wa jopo hilo la ICC kuwa na uelewa wa jinsi mfumo wa vyombo vya
mahakama vya utawala wa Kizayuni unavyofanya kazi.
Hapo kabla Mamlaka ya Ndani ya Palestina iliitaka Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai ichukue hatua ya kuchunguza jinai za kivita
zilizofanywa na utawala wa Kizayuni, hatua ambayo iliwafadhaisha mno
viongozi wa utawala huo ghasibu.
Mbali na Mamlaka ya Ndani, shakhsia mbalimbali wa
Kipalestina wamekuwa wakitoa wito wa kuchunguzwa jinai za kivita
zilizofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa
Gaza.
Mustafa Barghuthi, Katibu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya
Palestina alisema hivi karibuni kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
imekuwa ikisuasua katika kuchukua uamuzi wa kuanzisha uchunguzi kuhusu
vita vya Gaza.
Barghuthi alisisitiza kuwa kuna ulazima wa kufanyika
uchunguzi wa suala hilo na kuongeza kwamba haipasi kuiruhusu Israel
ijivue na mas-ulia na dhima ya jinai ilizotenda katika vita vya siku 50
dhidi ya Gaza.
Zaidi ya Wapalestina 2,300 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto
wadogo waliuawa shahidi na maelfu ya wengine walijeruhiwa katika
mashambulio ya siku 50 mtawalia yaliyofanywa na jeshi la utawala wa
Kizayuni mwaka 2014 dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Afisa wa ngazi za juu wa Iran amesema taasisi
za haki za binadamu zinataka serikali ya Saudi Arabia iwajibike, ilipe
fidia, na iwashtaki wale waliohusika na maafa ya Mina katika ibada ya
Hija mwaka jana.
Sayyid Mohammad Ali Husseini, Mshauri wa Masuala ya Kimataifa
wa Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa
Iran ameashiria maafa ya kuogofya ya Mina na hatua ambazo zimechukuliwa
na Iran ili kuhakikisha familia za waathirika wa maafa hayo wanapata
haki zao na kusema:
"Baada ya kupita mwaka mmoja tokea yajiri maafa ya
kuogofya ya Mina ambapo maelfu ya Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu
walipoteza maisha kidhalimu, serikali ya Saudia si tu kuwa haijawajibika
hata kidogo kutokana na maafa hayo, bali pia imezuia na imeweka vikwazo
na kuwazuia maelfu ya watu kutekeleza nguzo ya Kiislamu ya Hija mwaka
huu."
Husseini ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran ameongeza kuwa, hata kama tutakubali kuwa serikali ya Saudia
haikuwa imepanga kutekeleza kwa makusudi maafa ya Mina, lakini ilipaswa
kukubali kuwajibika kutokana na usimamizi wake mbovu.
Sikukuu ya Eid al-Adha ya mwaka jana ilishuhudia maelfu ya mahujaji
wa nyumba ya Mwenyezi Mungu wakiwemo mahujaji 464 wa Iran wakipoteza
maisha yao katika ibada ya Hija wakati wa kutekeleza ibada ya kumpiga
mawe shetani katika eneo la Mina.
Maafa hayo yalisababishwa na usimamizi
mbaya wa viongozi wa utawala wa Aal Saud. Baada ya kutokea maafa hayo
ya kusikitisha, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliitaja serikali ya Saudia
kwamba, ndio mhusika mkuu wa maafa hayo ya kutia uchungu na imekuwa
ikitumia mbinu mbalimbali za kisiasa na kisheria ili kuhakikisha familia
zilizokumbwa na msiba huo kutokana na maafa ya Mina zinapatiwa haki
zao.