Monday, September 28, 2015

Ban: Mgogoro wa Yemen hauwezi kutatuliwa kwa silaha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mgogoro wa Yemen hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi.
Ban Ki-moon ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. 
Amesema kuwa kwa sasa inaoneka kuwa, kupata fedha kwa ajili ya kuua watu katika nchi zao ni rahisi zaidi kuliko kupata fedha kwa ajili ya kuwalinda watu. Ban Ki-moon amesema kuwa mashaka na matatizo ya mwanadamu wa leo hayana kifani na kwamba kizazi kipichopita cha mwanadamu hakikukumbana na mashaka makubwa kama haya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kwa sasa watu milioni 100 wanahitaji msaada na wengine milioni 60 wamelazimika kukimbia makazi yao. Amesisitiza kuwa kwa sasa kuna udharura wa kupatikana utatuzi wa kudumu wa migogoro wa dunia.
Amesifu jitihada zinazofanywa na Ulaya kuwasaidia wakimbizi na akatoa wito wa kutafutwa njia zenye taathira zaidi katika uwanja huo.
Vilevile katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka wahusika wakuu katika eneo la Mashariki ya Kati kuchukua hatua za kukomesha mgogoro wa Syria.chanzo irib

Buhari ataka kuchunguzwa sababu za maafa ya Mina

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu sababu za maafa yaliyotokea Mina huko Saudi Arabia ambapo serikali ya Riyadh inalaumiwa kwa kushindwa kusimamia ipasavyo ibada ya Hija.
Rais Muhammadu Buhari ametoa salamu za rambirambi kwa familia za mahujaji waliofariki dunia katika eneo la Mina na ameitaka serikali ya Saudi Arabia kuchunguza sababu za maafa hayo na kuhakikisha hayakariri tena. Buhari ameeleza kusikitishwa sana na maafa ya Mina ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu wakiwemo mahujaji kutoka Nigeria. 
Rais wa Nigeria amesema maafa ya Mina hayazihusu nchi zilizopoteza mahujaji katika tukio hilo bali ni kadhia ya ulimwengu mzima wa Kiislamu. Buhari amemtaka Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba maafa hayo hayatokei tena.chanzo irib

Iran: Saudi Arabia imehusika na maafa ya Mina

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kufutwa kazi baadhi ya maafisa wa serikali ya Saudi Arabia kuhusu maafa yaliyotokea Mina wakati wa ibada ya Hija, hakutoshi.
Waziri Abdul Ridha Rahman Fadhli amesema kufutwa kazi baadhi ya maafisa waliohusika na maafa ya Mina hakutoshi na kwamba viongozi wa serikali ya Saudia wanapaswa kukabiliana na suala hilo la sasa kimantiki, kisheria na kwa njia zinazofaa ili waweze kufidia makosa yao ya huko nyumba.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, nchi kadhaa zimeafikiana na Saudi Arabia kuzika maiti za mahujaji wao mjini Makka lakini Iran inaendeleza jitihada za kurejesha nchini mahujaji wake wote wakiwemo wale waliotoweka na waliojeruhiwa, na Saudi Arabia inalazimika kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu katika uwanja huo.
 Amesisitiza kuwa, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini Ayatullah Ali Khamenei, Saudia inapaswa kukubali majukumu yake na kuuomba radhi Umma wa Kiislamu kutokana na maafa ya Mina na kuwachukulia hatua maafisa wote waliozembea katika maafa hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa mahujaji 169 wa Iran wameaga dunia, 295 wametoweka na 45 wamejeruhiwa.chanzo irib

Rais Kikwete kuzindua onesho la Utalii la Swahili International Expo

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (kulia) akizungumza Septemba 27, 2015  Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya onesho la Swahili International Expo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet Jimmy Kibati kama mmoja wa wadhamini.


ONESHO la Swahili International Expo linatarajiwa kufanyika wiki hii, kuanzia tarehe 1-3 Oktoba,2015 katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Hii ni mara ya pili kwa Onesho hili kufanyika,
Mwaka jana ilikuwa mara ya kwanza October 1- -4,2014
Onesho la mwaka jana liliweza kuwavutia Waoneshaji 40,Mawakala wa Utalii walioalikwa kutoka nje ya nchi 19 (hosted Buyers),Waaandishi wa Habari kutoka nje ya nchi 4 (media),Wageni waliotembelea onesho hilo 1,200,Wadhamini  40 na Mdhamini mkuu alikuwa Ethiopian Airlines
Mwaka huu Waoneshaji ni 100,Mawakala wa utalii na waandishi wa habari walioalikwa 43, Wageni wanaotegemewa kutembelea onesho 2,000,Wadhamini 41 na Wadhamini wakuu wamegawanyika katika makundi.
Kuna Platinum Category ambao ni Ethiopian Airlines – Mdhamini Mkuu (usafiri kwa ajili ya mawakala wa nje walioalikwa)
Pia kuna Gold Categoryambao ni Fast Jet Airline Limited, An’gata camps Ltd, FB cars Ltd, Gibbs Farm,Ramada Resort Dar es ssalaam, SAA North America, Seacliff Hotel, Sopa Lodges and Spicenet Tanzania .
Kwa upande mwingine kuna Silver category ambao ni Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Antelope Tours and Safaris, Azam Marine, Congema Tours and safaris Ltd, Fernandes Tours & safaris, Melau Tours & Safaris Ltd, Precision Air Services, Shirika la ndege la Qatar, Rwandair, Shirika la ndege la Afrika Kusini , Shidolya Tours & Safaris Ltd, Sun Tours &travel Lts and Shirika la ndege la Uturuki.
Wengine ni BougainvillaSafari Lodge, Ledgar Plaza Hotel, Cenizaro Hotels & Resorts, Emerald Collection Zanzibar, Essque zalu Zanzibar, Holiday Inn Dar es salaam, Kudu Lodge, Kunduchi bBeach Hotel, Manyara Wildlife safari Camp, Maru Maru Hotel, Mberesero Lodges & Tented Camps, Melia Zanzibar, Neptunes Hotels, New Africa Hotel, Ocean Paradise Resort & Spa, PlanHotel Hospitality Group, Protea Hotel Courtyard, Seacliff Court Hotel & Luxury Apartments, Seacliff Resort & Spa Zanzibar, Serena Hotel, Southern Sun Dar es salaam,  White Sands Hotel.
Black tomato, Boogle Woogle, Cultural Art Center,Chuo Kikuu cha Tumaini  Makumira .
Kwa upande mwingine kutakuwa na kitengo cha Hosted Buyers Programme ambapo Programme Maalum ya kuwatembeza mawakala wa Utalii katika maeneo Wageni hao watatembelea Zanzibar , Lake Manyara na Ngorogoro.Lengo ni kuona, kujifunza kuhusu utalii wa Tanzania, na kuonja (kuexperience ) ukarimu wetu.
Pia kutakuwa na kitengo cha Cultural Village ambalo ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya maonesho ambapo wajasirimali wadogo wataweza kuonesha bidhaa na huduma zao.
Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Tinga Tinga, Wachongaji vinyago, watengenezaji wa Sanaa mbalimbali, wanamitindo, vikundi vya burudani  muziki wa bendi na burudani (Utalii Band) na Kikundi cha utamaduni kutoka Chuo cha Tumaini , Arusha .Pia kutakuwa na Nyama Choma (wageni wataweza kupata vyakula vya kitanzania )
Kwa ujumla TTB inawataka watanzania watembelee onesho hilo kutokana na ukweli kwamba onesho la S!TE ni fursa ya kuhamasisha utalii wa ndani,Watoa huduma mbalimbali za kitalii watakuwepo, wataweza kutumia fursa hiyo kutoa maelezo kuhusu huduma zao na kuwahamasisha watanzania kutembelea maeneo ya kitalii (vikundi mbalimbali vitawea kuhamasika –wanafunzi, wafanyakazi nk)

Dr. Magufuli Awambia Chadema "Mpeni hiyo Power ili niwe Raisi wa Tanzania"


Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Samora  Manispaa ya Iringa wakati alipokuwa akiwaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.

Dk. Magufuli amesema “Nipeni kura za ndiyo bila kubagua vyama vyenu kwa kuwa nitakuwa rais wa Watanzania wote  wakati nikitekeleza majukumu ya  kuwatumikia watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo,  Hata wale wa CHADEMA huwa mnasema (Peoples Power) mpeni Magufuli hiyo Power ili awe rais wa Watanzania wote” .
 Dk. John Pombe Magufuli akizungumza zaidi na wananchi wa Manispaa hiyo amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kujenga mahusiano ya Kidiplomasia na mataifa mbalimbali ndiyo maana Tanzania ina mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani zikiwemo nchi jirani, 
Amesema kwamba mara atakapochaguliwa na kuwa kiongozi wa Tanzania atahakikisha anadumisha mahusiano hayo na kuifanya Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii  na Kisiasa. chanzo Fullshangwe