Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (kulia) akizungumza Septemba 27, 2015
Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya onesho la Swahili International Expo
linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka
huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa
kampuni ya fastjet Jimmy Kibati kama mmoja wa wadhamini.
ONESHO la Swahili International
Expo linatarajiwa kufanyika wiki hii, kuanzia tarehe 1-3 Oktoba,2015
katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi.
Hii ni mara ya pili kwa Onesho hili kufanyika,
Mwaka jana ilikuwa mara ya kwanza October 1- -4,2014
Onesho la mwaka jana liliweza
kuwavutia Waoneshaji 40,Mawakala wa Utalii walioalikwa kutoka nje ya
nchi 19 (hosted Buyers),Waaandishi wa Habari kutoka nje ya nchi 4
(media),Wageni waliotembelea onesho hilo 1,200,Wadhamini 40 na Mdhamini
mkuu alikuwa Ethiopian Airlines
Mwaka huu Waoneshaji ni
100,Mawakala wa utalii na waandishi wa habari walioalikwa 43, Wageni
wanaotegemewa kutembelea onesho 2,000,Wadhamini 41 na Wadhamini wakuu
wamegawanyika katika makundi.
Kuna Platinum Category ambao ni Ethiopian Airlines – Mdhamini Mkuu (usafiri kwa ajili ya mawakala wa nje walioalikwa)
Pia kuna Gold Categoryambao ni
Fast Jet Airline Limited, An’gata camps Ltd, FB cars Ltd, Gibbs
Farm,Ramada Resort Dar es ssalaam, SAA North America, Seacliff Hotel,
Sopa Lodges and Spicenet Tanzania .
Kwa upande mwingine kuna Silver
category ambao ni Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,
Antelope Tours and Safaris, Azam Marine, Congema Tours and safaris Ltd,
Fernandes Tours & safaris, Melau Tours & Safaris Ltd, Precision
Air Services, Shirika la ndege la Qatar, Rwandair, Shirika la ndege la
Afrika Kusini , Shidolya Tours & Safaris Ltd, Sun Tours &travel
Lts and Shirika la ndege la Uturuki.
Wengine ni BougainvillaSafari
Lodge, Ledgar Plaza Hotel, Cenizaro Hotels & Resorts, Emerald
Collection Zanzibar, Essque zalu Zanzibar, Holiday Inn Dar es salaam,
Kudu Lodge, Kunduchi bBeach Hotel, Manyara Wildlife safari Camp, Maru
Maru Hotel, Mberesero Lodges & Tented Camps, Melia Zanzibar,
Neptunes Hotels, New Africa Hotel, Ocean Paradise Resort & Spa,
PlanHotel Hospitality Group, Protea Hotel Courtyard, Seacliff Court
Hotel & Luxury Apartments, Seacliff Resort & Spa Zanzibar,
Serena Hotel, Southern Sun Dar es salaam, White Sands Hotel.
Black tomato, Boogle Woogle, Cultural Art Center,Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira .
Kwa upande mwingine kutakuwa na
kitengo cha Hosted Buyers Programme ambapo Programme Maalum ya
kuwatembeza mawakala wa Utalii katika maeneo Wageni hao watatembelea
Zanzibar , Lake Manyara na Ngorogoro.Lengo ni kuona, kujifunza kuhusu
utalii wa Tanzania, na kuonja (kuexperience ) ukarimu wetu.
Pia kutakuwa na kitengo cha
Cultural Village ambalo ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya maonesho
ambapo wajasirimali wadogo wataweza kuonesha bidhaa na huduma zao.
Baadhi ya bidhaa hizo ni kama
Tinga Tinga, Wachongaji vinyago, watengenezaji wa Sanaa mbalimbali,
wanamitindo, vikundi vya burudani muziki wa bendi na burudani (Utalii
Band) na Kikundi cha utamaduni kutoka Chuo cha Tumaini , Arusha .Pia
kutakuwa na Nyama Choma (wageni wataweza kupata vyakula vya kitanzania )
Kwa ujumla TTB inawataka
watanzania watembelee onesho hilo kutokana na ukweli kwamba onesho la
S!TE ni fursa ya kuhamasisha utalii wa ndani,Watoa huduma mbalimbali za
kitalii watakuwepo, wataweza kutumia fursa hiyo kutoa maelezo kuhusu
huduma zao na kuwahamasisha watanzania kutembelea maeneo ya kitalii
(vikundi mbalimbali vitawea kuhamasika –wanafunzi, wafanyakazi nk)
No comments:
Post a Comment