Thursday, September 22, 2016

"Ni aibu kwa Waislam kukosekana Wodi maalumu ya Wanawake wa Kiislam pindi wanapojifungua" Sheikh Swalehe

Sheikh Abdullatwifu Swalehe Mmoja Mmoja wa Masheikh na Mwalimu wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) akihutubia Waumini katika Maadhimisho ya Siku ya Sikukuu ya (Eid al Ghadir) Siku ya Kutangazwa rasmi Ali (a.s) kuwa Kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w)MasjidGhadir, Kigogo Post Dar es salaam.
"Ni aibu ni aibu katika jamii nzima ya Waislam Tanzania bamoja na kuhitalifiana Madhehebu zao zote ni aibu kukosekana Hospitali au Wodi maalumu ya kujifungulia Wakinamama (Wanawake wa Kiislam), wodi ya Kiislam,kukawa na Madokta ambao ni Kina mama maalumu kwa ajili ya kuwasaidia kina mama katika hali ya kujifungua, ni aibu.

Lakini leo kwamba mama wa Kiislam mjamzito tena mke wa Sheikh anaenda katika Hospitali anaesimamia suala lake ni Dokta Mwanaume ni jambo ambalo inauma sana ten asana ya kwamba wewe /  Sheikh unasimama kila siku na unazungumzia maswala ya maadili,unazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu  Hukmu za Kisheria ili kesho na kesho kutwa mke wako anaenda Hospitali na anazaliwa na Dokta Mwanaume".Sheikh Swalehe
Na.Sheikh Abdullatwif Swalehe