Sunday, December 21, 2014

UMIHIMU WA KUKUMBUKA KIFO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)


Viongozi mbalimbali kutoka Hawza Imam Jafar Swadiq chini ya Sheikh Hemed Jalala na Kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania Sayyed  Arif wakiongoza matembezi ya amani.

Tukio la kufishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) mbele ya jamii ni jambo geni sana, kana kwamba katika historia ya ulimwengu tukio hili halikutokea. Ingawa tukio la kuzaliwa kwa Mtume Muhammad limepokelewa kwa nafasi kubwa isiyo kifani.

Kwa hiyo, unaweza kuona hafla mbalimbali za kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zikifanywa Misikitini, Madrasani, Majumbani, na katika Mazawia mbalimbali.

Hili ni jambo jema sana, swali liliopo hapa ni, je, huyu afanyiwae haya yu hai mpaka sasa? Au amekwisha kufa? Ni kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) amekwisha kufa.

Ndio maana katika mwezi huu wa Safar Waislam katika maeneo mbalimbali duniani wamo katika huzuni na simanzi kubwa ya kukumbuka tukio la kufariki dunia Mtume wa rehema, Muhammad (s.a.w.w).

Hapa Tanzania Uongozi wa Chuo Cha Imamu Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala Unaadhimisha Maadhimisho ya Kumbukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ambaye alifariki dunia tarehe 28 Safar mwaka wa 11 Hijria katika mji mtakatifu wa Madina.

Uongozi Huo Unawataka Waislam Wote kuungana Pamoja katika kukumbuka kifo cha mbora wa daraja bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), ili kusadia kuishughulisha jamii ya kiislam katika kukuza maadili na mafundisho sahihi aliyofundisha Mtume Muhammad.

Katika kukumbuka kifo cha mtume uongozi umeandaa Matembezi ya Amani ambayo  yataanzia Karibu na Msikiti wa Kichangani, Magomeni Kichangani Hadi Viwanja Vya Pipo kilichopo Kigogo-Post Jijini Dar es salaam.Yakiwa na Ujumbe “Mtume katuachia Vizito Viwili Tushikamanenavyo”.

Uongozi unawataka Masheikh na Walimu kuihamasisha jamii ya kiislamu kukumbuka matukio muhimu yaliyotokea, ili kuimarisha umoja na mshikamano baina ya waislam na wasiokuwa waislam katika kuishi kwa amani na maelewano.

Pia tunawataka Waislamu wote kufuata mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlulbayt (Watu maalum wa Nyumba ya Mtume) , ili tuweze kufikisha ujumbe sahihi aliotuachia, katika kukuza dini na ushirikiano baina ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu.

Matembezi ya Amani "kumbukumbu ya kifo cha Mtume"

Wanafunzi wa Hawza (Chuo) cha Imam Jafar Swadiq wakiongoza msafara kwa kuimba nyimboza maombolezoya kifocha mtume Muhammad (s.a.w.w)

Viongozi mbalimbali kutoka Hawza Imam Jafar Swadiq chini ya Sheikh Hemed Jalala na Kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania Sayyed  Arif wakiongoza matembezi ya amani.

Hapa Tanzania Uongozi wa Chuo Cha Imamu Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala Unaadhimisha Maadhimisho ya Kumbukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ambaye alifariki dunia tarehe 28 Safar mwaka wa 11 Hijria katika mji mtakatifu wa Madina
Waumini wa dini ya kiislmu wakiwa katika maombolezo ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) wakiwa katika matembezi ya amani. na picha hizo mbili ni viongozi wakuu wa dini katika nchi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran.