Saturday, January 26, 2019

Serikali na Watanzania watakiwa Kuwa na Mfumo wa Malezi kukabili Swala la Usafi | Sheikh Kasonso

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso wa akitoa Khutba leo Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, huku akizungumzaiUsafi ni katika Imani ya Dini Tukufu ya Uislamu 

Na: Twalha Ndiholeye
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso ameitaka Serikali pamoja na Watanzania kama kweli wanania ya kuhakikisha Miji na chi kwa Ujumla kuwa katika hali ya Usafi ni lazima kujizatiti katika swala zima la Kuwalea Watanzania na watanzania kulea watoto wao katika swala zima la kupenda Usafi.

“Ili sisi tuweze kuwa wasafi katika Majiji yetu na Miji yetu, kitu cha kwanza cha kuangalia ni jambo la Malezi, leo unawza kumkuta Mtu mzima anakula ndizi barabarani kasha anatupa ganda ovyo, hii inamaanisha kwamba hivyo ndivyo alivyolelewa” Amewataka Sheikh Kasonso.

Sheikh Kasonso ametoa wito huo leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, imeyoswaliwa Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam alipokuwa anazungumzai Usafi ni katika Imani ya Dini Tukufu ya Uislamu.

Aidha Sheikh Kasonso amesema kuwa Swala la Malezi huwa inakuwa Tabia, tabia huwa inarithiwa na tabia huwa inaigwa hivyo lazima ianze harakati ya kuwalea watoto wetu kuanzia Majumbani mwetu na Shuleni ili kuweza kusaidia upatikanaji wa Usafi katika maeneo yetu.

“Mfumo wa Kimalezi tabia huwa inakuwa na tabia huwa inaritihishwa na tabia huwa inaigwa, hata sisi hapa tukitaka Dar es salaam yetu iwe safi na miji yetu kuwa safi nan chi yetu ya Tanzania iwe safi, ipendeze, ing’are kila kona ni lazima tuanze kuwalea watoto Majumbani mwetu, Mashuleni, tukiwalea itakuwa kama vile tunavyosifia Bara la Ulaya” Amesema Sheikh Kasonso.

Hatahivyo Sheikh Kasonso amewataka Watanzania na Serikali kuwa wasidhani tabia ya Usafi walionazo Bara la Ulaya na Majirani zetu kuwa ni swala limetokea wamejikuta wanalo sio hivyo bali ni swala la Mfumo wa Malezi walivyojilea katika swala la Usafi.

“Bara la Ulaya leo hii huwezi ukakuta hata chupa ya Maji taka iko barabarani au huweziukakuta chupa ya maji imetupwa barabarani bahati mbaya hapana, yale usifikiri yametokea kibahatimbaya hapana, bali ni Mfumo wa Malezi waliolelewa wenzetu, kwahiyo hata mtoto tayari anajua afanye nini, hata mkubwa amekuwa katika mazingira kama yale” Amesema Sheikh Kasonso.


No comments: