Wednesday, April 22, 2015

Wamjua Muhammad Baqir (a.s).

Sheikh Muhammad Yusuf, mwalimu wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s) akitoa hotuba juu ya Mazazi ya Mjukuu wa Mtume, Muhammad bin Ali Baqir (a.s), kumbukumbu hizo zimeandaliwa na Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s), Kigogo-Post,Dar es salaam.

Sheikh Abdullatwif bin Swalehe akiwa pamoja na mmoja wa Wazee wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a.s) katika kukumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) ambaye ni Muhammad bin Baqir (a.s)

Wanafunzi wa Hawzat Imam Jafar Swadiq (a,s) wakiwa katika hali ya furaha ya kukumbuka mazazi ya Muhammad bin Ali Baqir (a.s), Kulia ni Ramadhani Amri na pembeni yake ni Daudi Shabani


Hadhrat Muhammad bin Ali (a.s) alizaliwa siku ya Ijumaa ya Tarehe 1 Rajab mwaka wa 57 Hijiria katika mji wa madina.

Baba yake ni Imam Ali bin Hussein na  Mama yake ni Fatma bint Hassain (a.s), yeye ndie mtu wa kwanza katika kizazi cha Imam Ali (a.s) alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na Imam Ali (a.s) na Fatma bint Muhammad. (a.s)

Muhammad bin Ali Baqir (a.s) ni Imam wa Tano baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kufariki Dunia, ambaye ni mojawapo katika ahlulbayt wa Mtume waliotakaswa na kila aina ya uchafu na Mwenyezimungu (swt).