Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akiongea na Waandishi wa Habari katika hafla ya Futari ya Pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
WAISLAMU nchini wametakiwa kuishi karibu na jamii husasan kuwakumbuka
watu wenye ulemavu katika kipindi hiki
cha mfungo wa ramadhani.
Mbali na hilo, wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe na
kuwafariji watu wenye ulemavu ambao wanahitaji maalum.
Wito huo uliotolewa jana wakati wa hafla ya futari ya pamoja
na watu wenye ulemavu ilioandaliwa na msikiti wa Ghadir, kigogo Post, Dar es
Saalam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi, alisema ili dhana ya
uislamu ikamilike ni lazima kuwa karibu na jamii kwa kuijali kwa kuiongezea
amani na furaha.
“Uislamu si kufanya ibada tu bali ni kuitazama jamii
tunayoishi ni kwa namna gani tunaijali, tunaishinayo kwa amani jambo kubwa ni
kuhakikisha tunaipatie amani jamii yetu”alisema
Aliongeza kuwa katika
vitabu vya Quran aya nyingi zinazungumzia kufunya ibada na kufunga lakini nusu
ya Quran hiyo inazungumzia namna ya kuishi karibu na jamii.
NaibNaibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi alisema miongoni mwa mambo ambayo vitabu
hivyo vitukufu vinaonesha ni namna ya kuwajali watu na kwamba hiyo ndio hali ya
uislamu.
“Mtu ambaye anayempendeza Mungu ni yule ambaye anawafariji
watu wengi zaidi na kwamba mbele ya Mungu hakuna mkamilifu wala mtu bora wote ni sawa hivyo ndugu zangu walemavu
karibuni hapa na mjisikie nyumbani”alisisitiza.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kigogo, George Manyama,
alisema katika bajeti ya serikali ya mwaka huu imewakumbuka watu wenye ulemavu
kwa kuwaondolea kodi vifaa tiba.
Alisema kinachosubiriwa ni utekelezaji wa bajeti hiyo na
kwamba ni fursa kwa watu wenye ulemavu kuhakikisha wanapata mahitaji yao yote
maalum katika sekta ya afya.
“Mimi ni Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu katika
manispaa ya kinondoni hivyo ni wakati mzuri kuwataarifu kuwa kuna pesa
zinatolewa na manispaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu kuondokana na hali ya
umaskini na kaunza kujikimu”alisema.
Diwani huyo aliongeza kuwa katika fedha zilizotolewa na
manispaa hiyo ni zaidi ya sh.milioni 32 kwa ajili ya vikundi 36 ambapo kati yao
wapo watu wenye ulemavu.
Manyima alisema miongoni mwa changamoto katika utoaji fedha
hizo ni upungufu na kwamba licha ya manispaa kupeleka fedha hizo katika benki
kwa ajili ya mikopo kwa watu wenye ulemavu bado kuna masharti magumu ya
kukopeshwa.
“Ninashukuru uongozi wa msikiti huu kwa kuwajali na kuwathamni
watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika mkusanyiko wa pamoja kwa ajili ya
kubadilishana mawazo na kuwafariji ambapo misikiti mingi hawafanyi hivi kama mskiti huu nasema
nashukuru sana” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi
wilaya ya Kinondoni, Mussa Geuza, alisema hafla hiyo inasaidia kuwakutanisha
watu wenye ulemavu na kutambuana.
Alisema watu wenye ulemavu wanachangamoto kubwa ikiwemo
kujaliwa na kuthaminiwa na kwamba idadi kubwa wananyanyapaliwa na kwa utaratibu
ambao wanaofanya uongozi wa msikiti huo ni lakuungwa mkono.
Hawa ni baadhi ya Walemavu mbali mbali waliohudhuria katika Futari ya Pmoja iliyofanyika Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam |
“Hii ni fursa kubwa kwa sisi kutambuana na kufahamu taarifa
rasmi kuhusu watu wenye ulemavu katika maeneo tunamoishi hivyo ninashukuru sana
uongozi wa msikiti huu”alisema.