Sheikh Mkuu wa Tanzania Ithna Ashariyyah Abdallah Seif amewataka vijana kuto rudi nyuma katika kumsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Seif alisema
maadui wa Maulid hawajui radha na faida ya kukumbuka mazazi ya mbora wa viumbe Mtume
Muhammad (s.a.w.w).
Hayo alisema jana katika sherehe ya kukumbuka
mazazi ya Mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w), mskitini Ghadir,
Kigogo-Post, Dar es salaam.
Ameongeza kuwa Waumini wanatakiwa kuwa na moyo wa
kuvumiliana baina yao kwani Mtume (s.a.w.w) alikuja duniani kwa ajili ya kuwa
rehema kwa viumbe vyote.
Kwa uapnde wake Sheikh
Abdullatwif Issa Swalehe wa Hawza Imam Jafar amewataka
Waislam kujikita katika utafutaji wa Elimu, ili waweze kumtetea Mtume kwa
usahihi
Sherehe hizo zimeandaliwa na Hauza Imam Jafar
Swadiq, chini ya Sheikh Hemed Jalala, iliyopo kigogo-Post,jijini Dar es salaam.
Mtume Muhammad(s.a.w.w) alizaliwa tarehe 17
mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 570 H.D.
Baba yake ni Abdallah ibn Abdul mutwalib bin
hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia
kwa mtume Ibrahiim (A.S) Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi
bin zuhra bin kilaab. Alizaliwa katika mji wa makkatul mukarramah ulioko
katika nchi ya Saudi Arabia.
Waumini wa Kiume wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la shia, wakiwa makini kusikiliza historia na sifa za mtume Muhammad (s.a.w.w) pindi alipozaliwa na kazi alizofanya kwa walimwengu wote. |
Wanafunzi wa Hauza Imam Jafar Swadiq, wakiimba Qaswida za Kumsifu Mbora wa Viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w). |