Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habarileo jijini Dar es salaam |
Habari Kamili
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Jambo la Palestina ni
Jambo la Ubinaadamu, matatizo wanayowakumba ni kwa watu wote bila kujali dini
zao.
“Jambo muhimu la Paletina ni kuuwaunganisha Waislam
na Wakristo Duniani na kusema kuwa jambo la Palestina sio jambo la Kidini bali
ni jambo la kila mtu mpenda amani na utulivu na maelewano ya Kibinaadamu.” amesema
Sheikh Jalala.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati
akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo
huwadhimishwa kila siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Sisi kama Viongozi wa Dini tumeshaanza harakati kabambe
za kuwatembelea baadhi za Maskofu, Wachungaji, makanisani kwao lengo la
kuwatembelea Maskofu pamoja na Wachungaji ni kuleta Ukaribu na kuwafundisha
watanzania kwamba Uislam hausemi ya kwamba Mkristo ni Adui yetu, bali Uislam
unasema Mkristo ni ndugu yetu”amesema Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh Jalala amesema Qur’an imetamka waziwazi
kwamba watu waliokaribu mno na waislam ni wale waliuosema sisi ni wakristo.