Habari Kamili
Jambo ambalo wanayo
waislam wote duniani siku ya kumi au siku ya Tisa haya yanakuwa ni masiku ya
Muharam, masiku haya tunakumbuka kifo cha mmoja katika wajukuu wa Mtume
Muhammad (s.a.w.w). anaitwa Imam Hussein (a.s), bwana huyu Imam Hussein (a.s),
ni mjukuu wa Mtume alitoka na aliuwawa katika masiku kama haya.
Lakini niseme
yakwamba kuuwawa kwa Imam Hussein
(a.s) kama mjukuu wa Mtume nadhani na
Mtume Muhammad (s.a.w.w) naye vilevile amefariki, amekufa na amezikwa , kwanini
mnaiona huzuni hii, watu wamevaa nguo nyeusi mnazoziona katika matembezi haya. Hayo
ameyasema leo katika matembezi ya Amani ya kukumbuka siku aliyouwawa Imam
Hussein (a.s),mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).yaliyo anzia Msikitini wa
Kablastani hadi Jirani na Msikiti wa Khoja Shia Ithnasheriya Posta, Dar es
salaam.
Swala kubwa ni Ujumbe
aliokuwa ameubeba Imam Hussein(a.s), ujumbe huu naamini yakwamba ni ujumbe
mkubwa , na ujumbe alioubeba, ulikuwa ni Ujumbe wa Uwanaadamu, Imam Hussein
(a.s) kwenye kipindi chake ni kipindi ambacho, Uwanaadamu ulikiuwa
umesambaratika , utu ulikuwa hakuna , Imam Hussein (a.s) akaja katika
kumrudisha mwanaadamu, kuwa mawanaadamu anaheshima, kurudisha umoja wa
Wanaadamu.
Na moja ya mambo muhimu
sana ambayo ni mazuri kuyagusia haya na
ambayo Imam Hussein (a.s) hatosahauliwa hata siku moja na ambalo Watanazania leo wanalihitajia, Imam
Hussein (a.s), moja ya mambo muhimu aliyetoka kwa ajili yake ilikuwa ni kuienzi
amani, ni kuenzi maelewano, ni kuenzi mshikamano, ni kuenzi kusikilizana.
Imam Hussein (a.s) ametoka
kwa sababu kipindi chake watu walikuwa wanakaa pamoja , hii hali ya umoja
ilikatika, hali ya maelewano ilisambaratika , hivyo akatoka na ujumbe mkubwa wa
kuhakikisha kwamba katika nchi zile
amani inarudi, utulivu unarudi, busara inarudi, kuelewana kunarudi na akawa
yupo tayari hata watoto wake wadogo wauwawe, lakini ahakikishe nchi inakuwa na
amani,utulivu unakuwepo.
Na sisi Watanzania leo
hii tukikumbuka kifo cha Imam
Hussein(a.s) moja ya jambo kubwa ambayo ndio ujumbe wetu kwa watanzania wote
pasina kubagua dini zao, iwe ni waislam , iwe ni wakristo,iwe ni Mabudha na iwe
watu ambao hawana dini, Watambue yakwamba moja ya ujumbe tunaoubebe ni Ujumbe
wa kuhimiza amani, amani hii waliyonayo watanzania kwa miaka mingi, amani hii
ambayo ni tunu la taifa letu, ni tunu ya dini, bali asili ya Dini yenyewe ni
amani.
Na mimi naamini ya
kwamba dini zote za mungu, iwe ni Ukrito,uwe ni Uislam,uwe ni Uyahudi, hazikuja
kuleta kufarakana , hazikuja kuleta kugombana , hazikuja kuleta kuvutana. Bali
zimekuja kuleta maelewano, masikilizano na amani.
Watanzania kipindi hiki
cha uchaguzi watambue yakwamba kuienzi amani ndio dini, Wakristo na Waislam,
walitambue hilo, na wale ambao watashindwa au watashinda, kwenye vichwa vyao
waweke yakwamba sisi watanzania ni watu
tumezoea amani,ni watu tuiozoea maelewano ni watu tunaotambua Tanzania ni
kisiwa cha amani, na kwamba jambo la amani ni jambo la dini, na kwa ajili ya
jambo hilo Imam Hussein (a.s) ameuwawa kwa ajili yake, na leo tunalikumbuka
Mwisho niseme yakwamba
tujitokeze kwa wingi kupiga kura, kwa sababu ndio wajibu wetu wa kisheria nay
ale mambo yote ambayo yataondoa amani, yataondoa masikilizano, mambo hayo ni
Harram, (hairuhusiwi) kwa sisi watu wa dini kuyasogelea, na ni wajibu (lazima )
kuenzi kila jambo ambalo litahakikisha tunapiga kura , tunawachagua Viongozi,
tukiwa nchi bado imetuli.
Nnchi bado ni kisiwa cha amani, na tuangalie nchi za
wenzetu kwenye vitindi vya uchaguzi, kwenye vitindi vya kampeni mazingira yao
ni magumu na amani yao imetoweka , amani iwe juu ya Imam Hussein (a.s)
aliyetoka kwa sababu ya kuienzi, umoja na Ubinaadamu na maelewano. Asanteni
sana.
Na:
Sheikh Hemed Jalala, Mmoj wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la
Shia Ithnasheriya Tanzania.