|
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akizungumza mbele ya Masheikh na Maimam katika Semina ya Maimam na Masheikh kuhusu kadhia ya Palestina.Pembeni yake ni Sheikh Khalfan Khamisi |
Waumini wa
dini pamoja na viongozi mbalmbali katikia nchi zote duniani wametakiwa
kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na kutengwa na
mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita
iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam
dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania Shekh Hemed Jalala wakati wa semina
ya maimam na mashekh kuhusu QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi
wa taifa la palestina na mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo
yamekumbwa na machafuko makubwa kipindi cha karibuni.
Aidha amesema
kuwa Palestina ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa
duniani,na ni alama ya dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku
akisema kuwa ndani ya taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa
wapelestina ni dhuluma kwa dini zote wakristo pamoja na waislam.
“Amesema
kuwa kwa sasa ni wajibu mkubwa wa viongozi wa dini na wapinga dhuluma kote
nchini kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea
katika mataifa hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya
umuhimu wa taifa la palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla”amesema
Sheikh Hemed Jalala..
Semina
hiyo ambayo imewakutanisha maimam pamoja mashekh mbalimbali kutoka Madhehebu
Tofauti ndani ya Uislam imefanyika Jijini Dar es salaam kwa kuandaliwa na
Tanzania thnasheriya Community pamoja na Hawzat Imam swadiq kilichopo kigogo
post jijini Dar es salaam.
|
Masheikh na Maimam kutoka madhehebu mbalimbali katika Uislam waliohudhuria katika semina hii. |
Akizumgumzia
malengo ya kufanyika kwa semina hiyo kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam
dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania shekh Hemed Jalala amesema kuwa ni
kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa wajue kuwa Taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo Amani
lakini wanaikosa hivyo watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na
kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia.