Monday, June 29, 2015

Jamii ielezwe Umuhimu wa Nchi ya Palestina-Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akizungumza mbele ya Masheikh na Maimam katika Semina ya Maimam na Masheikh kuhusu kadhia ya Palestina.Pembeni yake ni Sheikh Khalfan Khamisi
Waumini wa dini pamoja na viongozi mbalmbali katikia nchi zote duniani wametakiwa kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na kutengwa na mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita iliyodumu kwa muda mrefu sasa.


Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania Shekh Hemed Jalala  wakati wa semina ya maimam na mashekh kuhusu QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi wa taifa la palestina na mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo yamekumbwa na machafuko makubwa kipindi cha karibuni.

Aidha amesema kuwa Palestina ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa duniani,na ni alama ya dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku akisema kuwa ndani ya taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa wapelestina ni dhuluma kwa dini zote wakristo pamoja na waislam.

“Amesema kuwa kwa sasa ni wajibu mkubwa wa viongozi wa dini na wapinga dhuluma kote nchini kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea katika mataifa hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla”amesema Sheikh Hemed Jalala..

Semina hiyo ambayo imewakutanisha maimam pamoja mashekh mbalimbali kutoka Madhehebu Tofauti ndani ya Uislam imefanyika Jijini Dar es salaam kwa kuandaliwa na Tanzania thnasheriya Community pamoja na Hawzat Imam swadiq kilichopo kigogo post jijini Dar es salaam.
 
Masheikh na Maimam kutoka madhehebu mbalimbali katika Uislam waliohudhuria katika semina hii.
Akizumgumzia malengo ya kufanyika kwa semina hiyo  kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania shekh Hemed Jalala amesema kuwa ni kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa wajue kuwa  Taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo Amani lakini wanaikosa hivyo watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia.

No comments: