Friday, August 14, 2015

Aliyevamia stakishari ajisalimisha polisi mwenyewe

Wakati jeshi la polisi nchini Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam wakiendelea na msako mkali kuwasaka wale wote waliohusika na mauaji ya askari katika kituo cha polisi cha STAKISHARI,Hatimaye mtuhumiwa mmoja ambaye alikuwa anatafutwa na polisi kwa kuhusiaka na tukio hilo amejisalimisha makao makuu ya jeshi la polisi akiambatana na familia yake.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kamishna wa polisi wa kanda hiyo SULEMAN KOVA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA,ambapo amesema kuwa mtuhumia huyo alijisalimisha makao makuu ya jeshi la polisi akiwa na wake zake wawili baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa anatafutwa kwa hali na mali na jeshi la polisi.

Katika Taarifa ya polisi wakati wakielezea mafanikio ya polisi kuhusu tukio hilo iliyotoka terehe 20 mwezi wa saba ilimtaja ndugu ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA kama mmoja wa vinara wa tukio lile .
Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa msaidizi mkuu namba mbili wa kiongozi wa kundi hilo lililovamia kituo cha polisi stakishari tarehe 12 mwezi wa saba anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.

Aidha katika msako wa polisi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wengine wawili waliohusika na tukio lile ambao wametajwa kwa majina kama—
1-RAMADHAN HAMIS miaka 18 mkazi wa Mandimkongo
2-OMARY OMARY AMIRI miaka 24 mkazi wa mbagala.

Jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao

Maalim SEIF akutana na Viongozi wa CUF – ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi
wa CUF pamoja na wagombea uwakilishi na ubunge wa Chama hicho Wilaya za Unguja
katika ukumbi wa majid Kiembe Samaki.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wanancfhi CUF, Mhe. Maalim SeifSharif Hamad amesema upepo wa kisiasa Zanzibar unakivumia vyema chama hicho na matarajioni kupata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kutokea wa asilimia 80 katikauchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
 
Maalim Seif amesema hayo jana alipokuwa akiwahutubia viongozi
wa Wilaya na majimbo wa chama hicho huko Kiembesamaki, ambapo pia alitangazatimu itakayo kiongoza chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi mkuuuliopangwa kufanyika Oktoba 25.
 
Maalim Seif amesema kwa namna wananchi wanavyokikubali chamahicho na namna kilivyojipanga na iwapo kila kiongozi na mwanachama atatekelezamajukumu yake bila ya kulalamika kitachukua idadi kubwa ya majimbo ya uchaguzina kushinda nafasi ya Urais kwa kishindo.
 
“Mazingira yaliyopo Zanzibar ni mazuri sana kwa CUF kupata
ushindi ambao haujawahi kutokea, hivyo kila mmoja wetu aongozwe na dhamira yakuchukua nchi mwaka huu, na mara hii haibiwi mtu kura yoyote”, alisema Maalim
Seif.  
 
Alisema malengo ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni
kuwa na idadi ya kutosha ya majimbo yatakayo kiwezesha kufanikisha kikamilifumipango yake ya kuwaletea matumaini na maisha bora Wazanzibari chini yaSerikali ya Umoja wa Kitaifa.
 
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na wagombea waliopitishwana chama kwa upande wa Unguja, Maalim Seif amemtangaza Naibu Katibu Mkuu wa CUFZanzibar, Nassor Ahmed Mazrui kuwa ndiye Meneja wa Kampeni za Urais wa Zanzibar,akisaidiwa na mshauri wake wa Mikakati, Mansour Yussuf Himid.
 
Kaimu Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, akinukuu baadhi ya vifungu vya
katiba ya chama hicho vilivyoipa uhalali  Kamati tendaji ya chama hicho Taifa kufanya
uteuzi ya wagombea katika majimbo yaliyoongezwa kulingana na hali halisi
ilivyokuwa.
Aidha kwa upande wa Pemba, Maalim Seif alisema Mratibu wa
kampeni hizo ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi, Hamad Masoud Hamad akisaidiwana Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.
 
Maalim Seif alisema Zanzibar hakuna hata jimbo moja ambalo
chama hicho kinaweza kusema kwamba hakina matumaini ya kushinda na kwamba sualala kushinda au kutoshinda litategemea chama hicho kimejipanga vipi kuchukuaushindi.
 
Katibu Mkuu huyo wa CUF ameonya kuwa huu si wakati wa viongozina wanachama kuvutana na wala si wakati wa kukumbatia ubinafsi kwa baadhi yaokupeana majukumu wasiyo yamudu kwa kwa kuzingatia urafiki au ujamaa.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Ismail Jussa Ladhu alisema CUF
katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu CUF kitakuwa na kampeni ya aina yake kwamakusudi ya kuwathibitishia Wazanzibari na nchi nzima kuwa kweli kimejiandaakuiongoza Zanzibar.
Jussa alisema Agosti 22 wagombea wote waliopitishwa na chama
kugombea Uwakilishi watakwenda kuchukua fomu Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwasherehe kubwa ili kila mtu apate habari kuwa safari ya chama hicho kuiongozaZanzibar na kutimiza matarajio yao i imezna rasmi.
“Siku hiyo wagombea wote wa Uwakilishi Zanzibar watakwenda
kuchukua fomu, mwenye kupiga dufu, mwenye kupiga mbwa kachoka, mwenye kupiga
rusha roho ni ruhusa kufanya sherehe hizo”, alisema Jussa.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwa upande wa nafasi ya
Urais wa Zanzibar, ambayo mgombea wake ni Maalim Seif Sharif Hamad atakwenda
kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Agosti 23, ambapo pia chama hichokimeandaa shamra shamra za aina yake. 
Katika mkutano huo, Maalim Seif aliwakabidhi viongozi waWilaya na majimbo seti 40 za jezi kwa kila jimbo moja pamoja na mipira 120.

Serikali yajenga vituo 22 vya kutolea huduma za makataba

Serikali imejenga vituo 22 vya kutolea huduma za makataba katika Mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuimarisha mfumo wa kutoa elimu kwa wananchi.
Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mipango toka Bodi ya Huduma za makataba (BOHUMATA) Bw. Comfort  Komba wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Komba amesema kuwa huduma za maktaba zimefika katika Mikoa 22,Wilaya 19 na tarafa 2 ikilinganishwa na vituo 17 vilivyokuwa Mikoani na 15 katika Wilaya mwaka 2005.
“BOHUMATA imeshirikiana na Halmashauri za Wilaya za Ruangwa,Chunya,Masasi,Mbulu na Ngara katika kuanzisha na kuimarisha Maktaba Mpya katika Halmashauri hizo.” Alisisitiza Komba.
Aliongeza kuwa uanzishwaji wa maktaba  katika maeneo mbalimbali hapa nchini umesaidia kuongeza na kuhamasisha utamaduni wa kujisomea miongoni mwa wanajamii ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kuanzishwa kwa maktaba hizo .
Akitaja mafanikio mengine Komba amesema ni ongezeko la kiwango cha elimu,maarifa,taarifa na ujuzi miongoni mwa  wanajamii .
Pia Komba alitoa wito kwa watanzania na wasio watanzania kujenga utamaduni wa kutumia maktaba za umma kwa kuwa zipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote.
Bodi ya Huduma za maktaba Tanzania (BOHUMATA)  ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 6 mwaka 1975 ikiwa na jukumu la kuanzisha,kusimamia,kuongoza,kuimarisha,kutunza na kuendeleza maktaba za umma ili kujipatia elimu,maarifa,taarifa,mbalimbali zitakazowasaidia katika kujiletea maendeleo.

Angalia Kikwete Akimzika Kisumo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM  Marehemu Mzee Peter Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Hosiana Kisumo Mke wa Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yake huko Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee Peter Kisumo yaliyofanyika kijijini kwake Usangi-Mwanga Mkoani Kilimnjaro.Chanzo:Fullshangwe