Kiongozi
Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala Amewataka
Watanzania, Waislamu na Wakritso kuwa na Umoja wa dini zote kwa kurudi katika
mafundisho ya Dini zao Quran na Injiri.
Sheikh
Jalala amesema hayo jana katika hafla ya Futari ya Maoja na Kamati ya Amani
Mkoa wa Dar es salaama, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya
Tanzania Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam
na kuwasisitiza Watanzania, Waislamu na Wakristo kudumisha amani, maelewano na
masikilizano kwa kuzilia Nafsi zao kwa kumtambua Mwenyezi Mungu vizuri pamoja
na Vitabu vyao.
“Katika tunu
tunaoililia leo katika nchi yetu ya Tanzania nchi ya watu ambao ni wamaoja,
wamekuwa wanaishi pamoja bila kubaguana hata siku moja, wala hawajuani kwa
makabila yao, Umoja wa Dini zote ziliopo nchini Tanzania na dini kubwa
tulizonazo ni Uislamu na Ukristo, naamini ya kwamba Waislamu na Wakristo
wanaweza kuwa kitu kimoja watakaporudi kwenye Vitabu vyao Quran na Injiri vinasemaje”
Alisema Sheikh Jalala
Nae Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Issa Rwechungura
amesema baadhi ya Wafuasi wa dini ya Kiislamu wamekuwa hawafuati muongozo wa
dini ya Kiislamu na hatimae kuwa chanzo cha mifarkano katika Jamii inayowazunguka.
“Tunalazimika
kufuata Muongozo wa Dini ya Kiislamu baada ya kuwa tumesilimu, tatizo ndugu
zangu ni kwamba baadhi yetu katika waislamu hatuambatani na muongozo wa Dini ya
Kiislamu na matokeo yake inatokea Mifarakano kati yetu au kati yetu na
wasiokuwa Waislamu, kinyume kabisa na mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)”
alisema Sheikh Rwechungura.
Sheikh
Rwechungura amesema kuwa swala la makundi katika jamii yetu ni jambo ambalo
lipo na haliepukiki, bali wajibu wetu ndani ya jamii hususani ya Kitanzania ni kutafuta muafaka wa
kuishi kwa amani ili amani hiyo ituwezeshe kutekeleza majukumu yetu ya kirofo na
ya Kijamii.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Bukhar Foundation Sheikh Khalifa Khamisi akiongea katika hafla ya futari ya pamoja na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaam, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam. |
Hatahivyo
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Bukhar Foundation Sheikh Khalifa
Khamisi amewataka Watanzania kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani kupeleka
mawazo na akili kwa wenzetu Wapalestina kwani kwani hawapo katika amani na
utulivu.
“Ili tuishi
kwa usalama tunaweza kujifunza zaidi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
Watanzania na Waislamu kwa ujumla sote tupeleke akili zetu na mawazo yetu kwa
wenzetu wapalestina, Taifa la Palestina ni taifa ambalo limetekwa,
limechukuliwa na Mazayuni (Mayahudi) imewadunisha na kuwadhalilisha Waislamu,
Wakristo na Wapalestina wanaoishi katika taifa hilo, wakati sisi tuko hapa
katika hali ya amani tukilindwa na askari ambao hawana silaha, wenzetu
Wapalestina, Waislamu na Wakristo waishio Palestina wanazungukwa na askari
wenye silaha na anaepinga amri anauwawa” Amesema Sheikh Khamisi
Sheikh
Khamisi amesema kuwa moja ya leongo la Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni ili
mwanadamu aweze kusalimika na Vishawishi vya Mwili, uweze kuwa na udhibiti tama
za mwili na ili muweze kujifunza namna bora zaidi ili Watu waishi kwa Amani.