Kiongozi Mkuu wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala,akiongea na Wanahabari punde baada ya kumaliza hotuba yake. |
Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania amwevitaka Vyombo vya Habari kusimamia vitu muhimu vyenye
maslahi kwa Taifa pamoja na kutanua fikra na mitazamo kwa Jamii ambayo itapelekea
maendeleo nchini.
“Wanahabari wanatakiwa kuwa chanzo cha kuleta
mabadiliko mema katika jamii, pamoja na kuwaunganisha watanzania kuwa kitu
kimoja katika Nyanja za Kiuchumi, Kijamii, Kidemokrasia, hususani nchi
kuibakiza katika Amani” amesema Sheikh Jalala.
Shekhe Jalala
amekemea suala la Waislam na Watanzania kuwa na
fikra za kukufurishana na kunyosheana
vidole vibaya pamoja na kuitana majina mabaya (makafiri) kwani kufanya hivyo ni kuisambaratisha jamii na matokeo yake ni kuleta uvunjifu wa
amani.
Hayo
ameyasema leo katika semina maalumu ya Wanahabari yenye kauli mbiu “Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika Kuelimisha Jamii” iliyoandaliwa na Chuo Cha
Kidini cha Imam Swadiq, Kilichopo Kigogo-Post, Dar e salaam.
Amesema Kuwa
diniya Kiislamu haina mahusiano na uvunjifu wa amani ,kwani uislamu aliofundishwa
na Mtume pamoja na Mafunzo ndani ya qur’an ni Uislam ambao unaolingania amani,
maelewano,ushirikiano kwa dini zote.
Shekhe Jalala ameitaka jamii ya kiislamu kuyaelewa
na kusoma vizuri namna mtume alivyoishi ishi maka na madina kwani aliishi na
washirikina na mayahudi kwa amani na salama hivyo hivyo alikaa nao vikao ili
kulinda amani.
Hawa ni baadhi ya Wanahabari walioshiriki katika Semina ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika Kuelemisha Jamii. |
Hatahivyo amesema
kuwepo kwa bidii, jitihada na mikakati
ya dhati kwa viongozi wa dini wa
Tanzania itakuwa ni kiashirio kizuri cha amani kwa kuweka vikao vya pamoja kwa
mashekhe, maskoofu na wachungaji juu ya kulinda amani na si kukutana kwenye vikao
vya posho.
No comments:
Post a Comment