Tuesday, November 27, 2018

Matembezi ya Kukumbuka Kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) ni Kuonyesha Huruma ya Mtume”-Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa moja ya lengo la kufanya Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya Huruma tuwenayo Binadamu Tanzania na Dunia kwa Ujumla.

“Matembezi haya ya Amani ya kukumbuka Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuweza kuieneza katika mitaa yetu na Sehemu zetu na Tanzania kwa ujumla, kwani Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliletwa kwa watu wote na sio kwa watu Fulani tu” alisema Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alisema hayo jana katika Matembezi ya Amani (ZAFA) YA Kukumbuka Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu T.I.C pamoja na Hawzat Imam Swadiq Kigogo Dar es salaam.

Sheikh Jalala alisema kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) anafundisha huruma kwa watu wote bila kujali tofauti za dini,tofauti za madhehebu, tofauti za Kifikra na Kimtazamo, na tofauti za Rangi na Taifa.

“Mitaa hii ya Kigogo imejaa watu wenye dini tofauti, watu wenye madhehebu tofauti, watu wenye mitazamo tofauti, watu wenye rangi tofauti, matembezi haya ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kumuunga Mkono Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwamba yeye aliletwa kwa ajili ya watu wote”.

Aidha ametataka Viongozi wa dini ya Kiislamu, Kikristo, Wanasiasa na Viongozi wa Serikali kujenga mazoea ya kuwatembelea Wananchi wao bila kujali tofauti za hali ya Kimaisha pamoja na Kipato walizonazo wananchi wao kwani kufanya hivyo ni kumuenzi mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.w).

“Matembezi haya ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya waziwazi ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliingia Mitaani, kukutana na watu, kukutana na watu wa kawaida, kukutana na watu amabo sio matajiri na wala sio watu wenye uwezo mkubwa, malengo makubwa ni kuwaleta watu pamoja na kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja bila kuwabagua dini.”

Kwauapande wake Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikh Ramadhani Mwelekwa amewataka Watanzania kuendelea kuwa na Umoja na Mshikamano kwani kufanya hiyo ni kuenzi Mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu akiwemo Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Nabii Issa/ Yesu Kristo.

“Waislamu wote na wale hawajabahatika kuwa waislamu tumeungana kwa ajili ya kuonyesha Umoja na mshikamano ambao ndio lengo la kutumwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunafurahiya wote bila kujali itikadi zetu za kimadhehebu na wale ambao mnatuona Mitaani lengo kubwa ni kufikisha Ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa watu wote na Ulimwengu wote

Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo, Wanasiasa na Viongozi wa Serikali Tusije Tukalaghaiwa, Umoja tulionao Watanzania tukausambaratisha” Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala ameataka Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo, Wanasiasa pamoja na Viongozi wa Serikali kudumisha na Kuenzi UMOJA huu tuliyonao Watanzania pamoja na kuwataka kutolaghaiwa tukafikiwa mahala Umoja huu ukasambaratika.

“Jambo Muhimu tuondoke nalo, Kikao kinachoweza kuwakusanya Waislamu Shia Ithnasheriya, AhlulSunna, Maibadhi,Wasiokuwa Waislam Wakristo, Mayahudi hili ni jambo la kuenziwa, Waislam, Wakristo na Wanasiasa ambao mpo katika Jukwa Kuu, tusije tukalaghaiwa, tukafikia mahala umoja huu wa Kimadhehebu, Kidini na wa Kitanzania ambao ndio sababu ya utulivu huu unaouona na kujivunia huku tulikokuanako ni jambo la kuenziwa na Masheikh, Maskofu, Wanasiana pamoja na Viongozi wa Nchi” Alisema Sheikh Jalala

Sheikh Jalala alitoa wito huo jana katika Hafla ya Kusheherekea Kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, iliyofanyika Jana chini ya Usimamizi wa Jumuiya ya Waislamu T.I.C Pamoja na Hawzat Imam Swadiq , Iliyofanyikia jana katika Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam.

Kwa upande wake Mhe. Ali Mkomwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe akiongea kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo aliwataka Waislamu pamoja na Watanzania kudumisha Amani na Umoja wa Waislamu.

Jambo la Kwanza Mhe.Waziri alichoniagiaza ni swala la Amani, ili tuwehuru katika kufanya Ibada zetu na mambo yetu,kuna watu leo hawapendi kuona utulivu huu uliopo, jambo la pili aliloniambia niseme ni Umoja wetu wa Kiislamu, na kwa bahati nzuri Sheikh Alhad amelizungumza kwa upanda sana” Alisema Mkomwa

Nae Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa amesema Swala ya Umoja wa Kiislamu ni Jambo muhimu Sana na kuwataka Waislamu Kushirikiana kwa yale wanayokubaliana na kwa yale hatukubaliani tusilazimishane ambapo ndio chanzo cha uvunjifu wa Amani na Utulivu tulionao.

“Sheikh Jalala, Mimi siku zote utambulisho wangu ni wa Umoja wa Kiislamu, sitoweza kuwa Shia Ithnasheria nitaendelea kuwa AhlulSunna, nay eye Sheikh Jalala hawezi kuwa AhlulSunna ataendelea kuwa Shia Ithnasheriya, Jambo la Muhimu ni Umoja wa Kiislamu kama hapa tulivyokaa, Masheikh wa AhlulSunna na Masheikh wa Shia Ithnasheria na Watoto wetu tunamsheherekea Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika yale tunayokubaliana tunakuwa pamoja, tusiokubaliana tunaachana tutakutana akhera shida iko wapi?” Alisema Sheikh Alhad Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hatahivyo Nae Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe. Ali Mtulia amemtaka Sheikh Jalala kuendelea kufanya kazi za Kijamii badala ya kujikita tu katika mambo ya Dini pekee, ambapo ndio miongoni mwa kazi alizokuwa anafanya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ndio Kiigizo chetu.

“Sheikh Jalala nakushukuru sana kwa hadhara hii nzuri, nimeonana na wapigakura wangu wa Kinondoni, lakini nikuombe Sheikh Jalala,alikuwa Kiongozi wa Dola yake, lakini alikuwa anafanya Shughuli za Kijamii, akikusanya zaka, wakitoa Sadaka, wakifanya mambo ya Tiba, wakifanya Mambo ya Mahusiano, wakitoa na Ushauri, Sheikh wangu Sheikh Jalala, nakukabidhi Kata ya Kigogo uendelee kufanya Mambo ya Kijamii” Mbunge wa Mtulia