Sunday, June 18, 2017

Sheikh Jalala awataka Viongozi wa Dini kuwalinda Vijana na Ugaidi

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vijana wa Kata ya Kigogo katika Futari ya pamoja iliyowakusaya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu, iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
Viongozi wa dini mbalimbali na serikali wametakiwa kuwa karibu na vijana ili wafundishwe  maadili mema wasije kuwa na fikra za ugaidi  baada ya kukata tamaa ya kukosa kazi. 

Wito huo ulitolewa jan Dar es Salaam na Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithanasheriya Tanzania, Sheikh Hemed Jalala, katika futari ya pamoja na vijana hao wa kiislam na wasiokuwa waislamu wa Kata ya Kigogo wakati  akizungumza nao kutambua lengo la uwepo wao.
 
Hawa ni baadhi ya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu wa kata ya Kigogo waliohudhuria katika Futari ya pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.
Sheikh Jalala, alisema vijana wa sasa wamejitenga na mambo ya kiroho wamekata tamaa ya maisha kwa kukosa kazi hivyo ni wajibu wa viongozi kuwa karibu nao kusikiliza changamoto zao.

"Vijana ni tunu ya taifa, ndio muhibili wa jamii kwani taifa ambalo halina vijana wenye maadili mazuri liko hatarini kuwa na vijana ambao wanaweza kujiingiza na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ugaidi.

Sisi kama viongozi ni wajibu wetu kuwa karibu nao kuwafundisha namna ya kuwa karibu na nyumba za ibada ili baadaye tuweze kuwa na vijana watakaoliendesha taifa letu la Tanzania,’’alisema.
 
Mwl. Kassim Hassan ambae pia ni Mdau wa mambo ya Kijamii kutoka shule ya Sekondari Kibondo akiwapa elimu vijana walioudhuria semina jana Kigogo jijini Dar es salaam.
Alisema vijana  watakapokuwa wamefundishwa kwamba Mungu ni mpenda amani  na kinachokubaliwa ni maelewano mazuri na sio ugaidi.

Hatahivyo Jalala, alisema dini ya kiislam haina mahusiano na masuala ya ugaidi ambayo ni kuuana na kuchinjwa kwani Uislam inafundisha Amani,mshikamano na maelewano kwa kila mtu.