Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemedi Jalala. |
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemedi Jalala amesema Uislaam si dini ya kutisha
watu, kuwafanyia watu ukatili,uislaam unavutia, muislaam ana haiba muislaam
muda wote amebeba amani,Muslaam ni Yule ukimuona hata usiku wa manane unahisi
upo katika amani.
Hayo ameayasema leo katika Swala Ya Ijumaa ya Mwisho
wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1436 iliyoswaliwa katika msikti wa Ghadiir-kigogo
Post Dar es salaam.
Jalala amesema
kuwa Mwislam ni Yule ambaye hana tabia ya kuwatukana watu, hana tabia ya
kuwagawa watu kwa ulimi wake hana tabia ya kusababisha fitna kwa watu wala hana
tabia ya kuwahusudu watu “ ukimpata mtu ana shughulika na hayo ujue si mwislaam,
mumtafutie dini nyingine.
Akizungumzia hatua za kuifikia amani, maulana alianza kwa aya katika Surat anfal :17“kama wasio waislaam watakua wanapenda amani nawe (Muhammad s.a.w.w)usiipinge amani hiyo, elekea katika amani hiyo na mtegemee mwenyezi mungu kwani yeye ndie mwenye kusikia na mjuzi
“Mara nyingi tuna hubiri amani kuwa ni tunu na kitu
cha kuenziwa, lakini kuna watu wana ufahamu mbaya kwa kudhani kua wanoihubiri
amani huenda ni vibaraka au wana tumiwa, hawajui kua amani ndio asili ya dini.
Kwani asili ya dini ni amani,maamkizi ya dini ni amani, anae ihubiri amani ndio
anaeihubiri dini si kibaraka”amesema Jalala
Akiinukuu hadithi ya mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema “Mbora wenu ni Yule anaewalisha watu chakula, aneieneza amani, na anaeswali usiku watu wakiwa wamelala.” Nae imam jaafar swadiq(a.s) mjukuu wa mtume (s.a.w.w) amesema :muislaam ni Yule watu wamesalimika nae kutokana na mikono yake na ulimi wake.
Aidha amesema kuwa tukitaka Tanzania iendelee kua kisiwa cha amani, tukitaka Dunia iwe ya Amani, hatua ya kwanza ni kumuheshimu binaadam mwenziokwani kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe, kupeana adabu ,mkishikamana itaondoka dharau na kuja amani,
Jalala amezitaka mataifa yanayojiita makubwa ya ulimwengu wa kwanza, lazima waondoe dharau na kiburi kwa watu wa ulimwengu wa tatu,inapasa wawaheshimu ili amani iweze kuendelea na kudumu duniani.
Hatahivyo amewataka waumini wa Kiislaam kutokubezana
na kuitana kwa majina yasiyofaa, kwani kufanya hivyo ni kuingiza mizozo na
mifarakano, na matokeo yake ni kukosekana kwa amani katika jamii na kwa Taifa
kwa ujumla.