Na: Twalha
Ndiholeye
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Muosa
Farhang amesema kuwa kitabu cha Shirazi na Baluchi ni kitabu kinachoonyesha
Uhusiano wa wazi na wa kihistoria kati ya Taifa la Tanzania na Taifa la Iran.
“Leo hii tunafuraha kubwa kwa uzinduzi wa Kitabu ambacho
kinaelezea historia ya Washirazi, Wabaluchi na Watanzania, kwa kuzingatia kwamba
uwepo wa Washirazi na Wabaluchi katika Tanzania kulikuwa na athari kubwa kwa
vizazi vijavyo” Balozi Farhang.
Balozi Farhang alisema hayo jana baada ya Uzinduzi wa Kitabu
hicho kilijulikanacho kwa jina la Shirazi na Baluchi, uzinduzi huo ulifanyika
katika kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jijini Dar es
salaam.
Aidha Balozi Farhang aliwataka Watnzania kuwa na uwelewa
sahihi juu ya uhusiano wa wazi na wa kihistora katika ya Taifa la Tanzania na
Taifa la Iran kwa kupitia Shirazi na Baluchi ambao walifika Tanzania kabla hata
ya Uhuru wa Tanzania na kuwa makini na wale wote wanaopotosha Historia hii.
“Uzinduzi huu wa Kitabu hiki ni sehemu tu ya utamaduni na
historia amabyo inabidi watanzania waelewe, na ninaamini itabaki kwa muda
mrefu,Napenda kuwaambia watanzania kuna historia ndefu na kubwa zaidi ambayo
iliyopita, ila nasikitika hii historia inaanza kupotea ambapo inadini sasa
historia ianzwe kurudiswa, bila shaka historian a utamaduni mkubwa walionao
watanzania inaweza kusaidia nchi zote za jirani, eneo la afrika mashariki”
alisema Balozi Farhang
Kwa Upande wake Muadishi wa kitabu cha Shirazi na Baluchi
Mhe. Charles Kayoka alisema kuwa kitabu hiki cha Shirazi na Baluchi kinaonyesha
Shirazi na Baluchi waliingia nchini kabla ya miaka 300 kwa Baluchi na 1000 kwa
Shirazi iliyopita.
“Kitabu hiki
kinazungumzia kwa ufupi historia ya Wabalunchi na Washirazi kama watu ambao
walikuja nchini zaidi ya miaka 300 wabalunchi na zaidi ya miaka 1000 kwa upande
wa Shirazi”
Charles Kayoka ambae pia ni Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam katika Idara ya Sanaa na Ubunifu alisema kuwa Kiatabu kinaonyesha
Ushahidi wa kuja kwao kwa ushahidi wa majumba na ushahidi wa watu ambao
wameshakuwa viongozi au nyumba za makazi ambayo waliwahi kuishi maeneo
mbalimbali, Picha za makazi ya watu na watu wenyewe zilitoka afrika mashariki
kama Mtwara, Lindi, Unguja na Pemba nchini Zanzibar, Tanga pamoja na Mombasa.
“Hichi
kitabu kwa sisi watanzania kinajaribu kuonyesha ni Taifa ambalo linahistoria
ndefu na pana, ambayo inatakiwa ichapishwe, nap engine kuangalia namna gani
historia hii itaendelea kutafitiwa zaidi, kwa ajili ya kuiboresha historia
yetu, ambapo kwa wale walioandika kunavitu vingi waliviacha, hii itatusaidia
sisi kama Watanzania”