Tuesday, June 6, 2017

Makamu wa Rais afanya ziara serengeti na haya ndio ameyasema

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mbuzi Mugumu Serengeti ikiwa sehemu ya kukamilisha ziara yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Serengeti na kuwapongeza kwa kutunza mazingira
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza kwenda kupata huduma afya.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo leo 6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya  na kuweka jiwe la msingi.

Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.

Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.

Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Korea Kaskazini inaandaa silaha ya kuifuta kabisa Marekani kwenye uso wa dunia

Gazeti rasmi la Korea Kaskazini la Minchu Chosun limeandika kuwa, hivi sasa Pyongyang inaendelea na maandalizi ya kuunda silaha yenye uwezo wa kuifuta kabisa Marekani kwenye uso wa dunia kutokana na Washington kuendelea kujizatiti katika eneo la Peninsula ya Korea. 

Taarifa ya gazeti hilo imewanukuu makamanda wa kijeshi wa nchi hiyo wakisema kuwa, hivi sasa Marekani inajiandaa kufanya shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini kupitia utumaji wa meli yenye uwezo wa kubeba 

Limeongeza kuwa, hatua hiyo ya Washington, inaifanya idadi ya meli kubwa za kijeshi za nchi hiyo zilizotia nanga katika pwani hiyo ya Korea kufikia tatu ikiwemo ya USS Ronald Reagan na USS Carl, suala ambalo linaifanya Pyongyang nayo ijiandae kukabiliana na hatari yoyote tarajiwa. 

Wakati huo huo, nyambizi ya Marekani yenye kubeba silaha za nyuklia pia imetia naga katika pwani ya Korea baada ya kumaliza kushiriki maneva ya kijeshi na Japan.

 Gazeti rasmi la nchi hiyo la Minchu Chosun limebainisha kwamba, Pyongyang inaendelea kulifanyia marekebisho kombora lenye uwezo wa kuisambaratisha Marekani iwapo Washington itajaribu kutekeleza hujuma yoyote dhidi yake.

Weledi wa masuala ya kijeshi eneo la Peninsula ya Korea wanaamini kuwa, maandalizi ya Marekani katika eneo hilo yanabainisha kwamba Washington imepanga kufanya mashambulizi dhidi ya Pyongyang. Hayo yanajiri katika hali ambayo Marekani imeiwekea Pyongyang vikwazo zaidi kwa sababu ya miradi yake ya nyuklia na makombora ya balestiki.

"Viongozi wa Dini Wapiganieni Wanyonge" Sheikh Alhad

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa akiongea jana katika Semina ya Mchango wa Imam Khomein (r.a) iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.ikiwa ni Maadhimisho ya Kifo chake Imam Khomein (r.a)
Habari Kamili


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, amewataka viongozi wa dini kutokuwa na ubaguzi na badala yake kuwapigania wanyonge ili  kupata haki zao.

Aidha, amewasihi viongozi hao kujitoa kama  Imam Khomein (r.a) ambaye alijitoa kwa ajili ya watu wote ulimwenguni na kwamba hakujitoa kwa ajili ya waislamu pekee wala Mashia, bali alijitoa kwa wanadamu kupata haki zao.

Wito huo ulitolewa jana Dar es Saalam wakati wa semina  iliyozungumzia mchango wa Imam Khomein (r.a) katika ulimwengu, ambayo iliyofanyika katika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar e alaam, Sheikh Alhad Mussa akiongea na Waandihi wa Habari jana alipohudhuria katika Semina ya Mchango wa Imam Khomein (r.a) iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.
“Historia haiwezi kumsahau Imam Khomein (r.a) bali ni lazima tuendelee kumkumbuka kwa sababu ni Kiongozi ambae ni mfano katika jamii, kwani alilingania umoja, haki, usawa na alipinga kila aina ya unyanyasaji na dhuluma katika jamii” alisema Sheikh Mussa.

Aidha,Sheikh Mussa alisema Imam Khomein (a.s) ni Kiongozi ambae ni mfano katika jamii kuna haja ya kuigwa mazuri yake na kwamba si bali alikomboa Mapinduzi ya Kiislam ya Iran, lakini pia alifanya mapinduzi ya kifikra.

“Imam Khomein (r.a) aliwakomboa watu waliodhulumiwa, alisimamia  haki na uadilifu katika jamii,kuhakikisha mnyonge anakuwa na haki duniani,’’alisema. 
 
Muanzilishi na Kiongozi wa  Kanisa la Ufunuo Tanzania Nabii Paulo Bendera akiongea katika semina hiyo.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo Tanzania, Nabii Paulo Bendera, alisema amejifunza mambo makuu matatu kutoka kwa Imam Khomein (r.a) ambayo ni usawa, haki na kuwatetea watu wanaonyonywa na wanaokandamizwa katika jamii.

Alisema Imam Khomein (a.s) alikuwa ni mtu wa watu, alikuwa anapenda haki, usawa na aliwatetea watu wanaonyonywa pamoja na kuwatumikia watu kwa moyo wa dhati,

“Nashukuru sana kwasababu ninajifunza mengi ndani ya dini ya Kiislamu, hata miezi iliyopita nilimkaribisha sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kanisani kwangu na nikampatia fursa ya kuhutubia na waumini walifurahi sana”alisema 

Aliongeza kuwa viogozi wa dini wanapaswa kuonyesha ushirikiano baina ya viongozi wa Kikristo na wa Kiislamu na kwamba ni wajibu kufungua nafasi zaidi ya upendo, mahusiano mema kati ya wakristo na waislamu.
 
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Semina hiyo.
Naye Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya waislamu wa Shia, Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala alisema kuwa uislam unatoa mafunzo ya kuishi vizuri na watu wote, pamoja na kuwa na moyo wa huruma.