Gazeti rasmi la Korea Kaskazini la Minchu Chosun
limeandika kuwa, hivi sasa Pyongyang inaendelea na maandalizi ya kuunda
silaha yenye uwezo wa kuifuta kabisa Marekani kwenye uso wa dunia
kutokana na Washington kuendelea kujizatiti katika eneo la Peninsula ya
Korea.
Taarifa ya gazeti hilo
imewanukuu makamanda wa kijeshi wa nchi hiyo wakisema kuwa, hivi sasa
Marekani inajiandaa kufanya shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini kupitia
utumaji wa meli yenye uwezo wa kubeba
Limeongeza kuwa, hatua hiyo ya
Washington, inaifanya idadi ya meli kubwa za kijeshi za nchi hiyo
zilizotia nanga katika pwani hiyo ya Korea kufikia tatu ikiwemo ya USS Ronald Reagan na
USS Carl, suala ambalo linaifanya Pyongyang nayo ijiandae kukabiliana
na hatari yoyote tarajiwa.
Wakati huo huo, nyambizi ya Marekani yenye
kubeba silaha za nyuklia pia imetia naga katika pwani ya Korea baada ya
kumaliza kushiriki maneva ya kijeshi na Japan.
Gazeti rasmi la nchi hiyo
la Minchu Chosun limebainisha
kwamba, Pyongyang inaendelea kulifanyia marekebisho kombora lenye uwezo
wa kuisambaratisha Marekani iwapo Washington itajaribu kutekeleza hujuma
yoyote dhidi yake.
Weledi wa masuala ya kijeshi eneo la
Peninsula ya Korea wanaamini kuwa, maandalizi ya Marekani katika eneo
hilo yanabainisha kwamba Washington imepanga kufanya mashambulizi dhidi
ya Pyongyang. Hayo yanajiri katika hali ambayo Marekani imeiwekea
Pyongyang vikwazo zaidi kwa sababu ya miradi yake ya nyuklia na
makombora ya balestiki.
No comments:
Post a Comment