Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
amesema kuwa, kukaguliwa vituo vya kijeshi ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran.
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya IranBrigedia Jenerali Hussein Dehqan |
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan ameelezea madai ya
uwongo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Magharibi likiwemo gazeti la
Guardian la Uingereza ya kukaguliwa vituo vya kijeshi vya Iran
ikiwa ni sehemu
ya makubaliano ya Lausanne nchini Uswisi na kusisitiza kwamba, kamwe
hayakufikiwa makubaliano kama hayo.
Brigedia Jenerali Dehqan amesisitiza kwamba, suala
la kukaguliwa vituo vya kijeshi hapa nchini, ni mstari mwekundu kwa Jamhuri ya
Kiislamu.
Hivi karibuni yalifikiwa makubaliano kati ya Iran na
kundi la 5+1 ambapo moja kati mafanikio makubwa iliyoyapata Iran kwenye
makubaliano hayo, ni kwa nchi hizo sita zenye nguvu duniani kuitambua rasmi
miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani.