Tuesday, January 14, 2014

Imarati yataka Iran iondolewe vikwazo

Umoja wa Falme za Kiarabu umesifu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na madola sita yenye nguvu duniani na kutaka kuondelewa vikwazo dhidi ya Tehran.

Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema kuwa Iran ni jirani ya Imarati na pande zote zitanufaika iwapo jamii ya kimataifa itaiondolea Iran vikwazo.

Uhusiano wa Iran na Imarati ni wenye umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili kwa kuzingatia kuwa makumi ya maelfu ya Wairani wanaishi huko Imarati.

Nchi hiyo inatumika kama njia kwa ajili ya miamala ya kibiashara kati ya Iran na nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi. 

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alifanya ziara nchini Imarati mwezi Disemba mwaka jana ili kuboresha uhusiano na nchi hiyo jirani ya Kiarabu na mshirika wa kiuchumi.
Chanzo irib


Sherehe za kusherekeakuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukumbuka mazazi ya Mtukufu wa daraja Mtume Muhammad (s.a.w.w)
Kuwakusanya watu kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kuitukuza sifa zake ambazo zimesifiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Nabii Isa (a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu amteremshie meza ya chakula, na siku hiyo ya kuteremshwa meza ya chakula akaitaja kuwa ni sikukuu:
"Ee Mwenyezi Mungu Mola wetu! tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu na kiwe ishara itokayo kwako, na turuzuku, kwani wewe ni mbora wa wanaoruzuku". 5:114.
Je. thamani ya kuwepo Mtume Mtukufu, ni ndogo kuliko meza ya chakula iliyotoka mbinguni ambayo Nabii Isa (a.s) ametangaza siku ya kuteremshwa chakula hicho kuwa ni sikukuu? Ikiwa kufanywa siku hiyo sikukuu ni kwa sababu chakula ilikuwa ni ishara ya Mwenyezi Mungu, Basi Je, Mtume Muhammad (s.a.w.w) si ishara kubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia rehema Mtume, na Malaika wake wanamteremshia rehema Mtume, enyi mlioamini! Muombeni rehema (Mtume) na muombeni amani". 33:56 iliposemwa Aya hii, Maswahaba waliuliza Mtume: Watamuombeaje rehema? Mtume akawafundisha, semeni: Allahumma swali a'laa Muhammad wa Aali Muhammad.