Tuesday, September 13, 2016

Sikukuu ya Eid haina maana kuvunja Sheria-Sheikh Abdi

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Abdallah Seif akiswalisha swala ya Eid Hajj jana katika Viwanja vya Pipo Kigogo Post Dar es salaam.

Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar es salaam wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Suleimani Serehani, pembeni yake ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) Sheikh Muhammed Abdu wakishiriki Ibada ya Swala ya Eid Hajj pamoja na waumini wengine.
 Shekh Mkuu wa jimbo la Dar es salaam la waislam Shia Ithna sheria Tanzania Shehk SULEIMAN SEREHAN, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid hajj katika Viwanja vya Pipo Kigogo jijini Dar es salaam, amesema  nchi ikiwa na amani na utulivu wananchi wake wanaweza kuswali na kufanya maendeleo ya kiuchumi pasina bugudha yoyote.

Sheikh Serehani amesema   kuwa amani ni kitu muhimu haswa kwa wakati huu nchi mbalimbali zinaingia katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.


Aidha kwa upande wake Naibu Mkuu wa chuo cha kislam(Hawzat) Imam Swadiq(a.s) Shekh MOHAMED ABDI ,amewataka waislam kusherehekea kwa kufata sheria za nchi zilizopo kuhakikisha hawaingilii na kuathiri shughuli za wengine.


Waislam wote wanasheherekea iddi kwa kukumbuka mambo mawili likiwepo la kuchinja kwa ajili ya kitoweo pamoja na kumtii mwenyezi mungu kwa mambo yote anayofanya.




Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Abadallah Seif akiongoza dua katika swala ya Eid Haji