Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Anna Henga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo hicho, Bw. Ezekiel Massanja |
KITUO
CHA SHERIA na haki za binadamu (LHRC) kimepongeza juhudi
zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kwa kupambana na mafisadi,
ikiwamo hatua ya kuundwa kwa kamati mbili za Rais zilizokuwa na lengo
la kuchunguza
thamani halisi ya madini yaliyomo katika makasha ya mchanga wa madini
(makinikia) na ile ya kuwafikisha viongozi waandamizi wa kampuni ya IPTL
mbele ya vyombo vya sharia.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
LHRC, Bi. Anna Henga amesema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hatua za
serikali ya awamu ya tano hususani katika suala zima la uwajibikaji na
usimamizi wa rasilimali za Nchi, na kusema wamebaini kuwa serikali
inapaswa kuungwa mkono ili vita hiyo ya uchumi iweze kufanikiwa.
Amesema
ukiangalia maamuzi makubwa yanayochukuliwa na Mh. Rais yote yamelenga
kurudisha hadhi ya Taifa ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi walio
wengi hivyo kuna kila sababu ya kuumunga mkono ikiwemo kutoa ushauri
mbalimbali.
“Ikumbukwe
mnamo Juni 9 mwaka 2017 kituo cha sharia na haki za binadamu kilitoa
tamko hapa mbele yenu kupinga kusudio la mamlaka ya udhibiti wa nishati
na madini (EWURA) kuiongezea muda wa kuzalisha umeme kampuni ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwa muda wa miezi 55” na
kuanzia hapo tulishuhudia hatua ambazo zilichkuliwa na serikali kama
kituo tunapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwapeleka mahakamani wahusika
wakuu wa kashfa ya Tegeta Escrow ambao ni zao la kampuni ya IPTL.
Amesema
hatua zinazochukuliwa sio tu zinaleta heshima katika Taifa lakini pia
zinarejesha Imani ya Watanzania kwa serikali yao kwani wanaona kumbe
dhana ya uwazi na uwajibikaji inawezekana na pia inafuta dhana ambayo
imejengeka kuwa viongozi wanalindana.
Licha
ya kuwepo kwa pongezi hizo lakini kituo cha sharia pia kimetoa angalizo
kama kweli tunahitaji kuwa na vita ya uchumi yenye mafanikio katika
Taifa la Tanzania lazima yafuatayo yakafanyika.
…YAKUMBUSHA YAFUATAYO KUFANYIKA
Kuundwa kwa mamlaka kamili ya madini; Kituo
cha sharia na haki za binadamu kimeishauri serikali kuunda Mamlka
kamili ya Madini itakayokuwa inafanya kazi ya uratibu wa shughuli zote
za madini Tanzania kama zilivyo Mamlaka ya hifadhi ya Jamii. Mamlaka
ambayo itakuwa na dhima ya kushughulika na mikataba yote ya madini,
mapato ya madini, kuidhinisha leseni (vibali), kuratibu soko la madini
ambapo madini yote yatauzwa hapa Nchini ili kupata fedha za kigeni.
Waliotajwa katika kamati zote mbili kuchukuliwa hatua, Pia
kituo kimeshauri kuwa wale wote waliotajwa katika ripote zote mbili za
Rais wachukuliwe hatua ikiwamo kuwafikisha katika vyombo vya sharia
kujibu tuhuma zao.
Waitaka bunge kubadilika Kituo
cha sharia kimetaka Bunge kubadilika kwenda sambamba na kasi ya
Serikali ya awamu ya tano, lisiendeshe mijadala kisiasa bali kwa lugha
za kibunge na kutanguliza maslahi ya Nchi mbele.
“Tumefika
hapa na kashfa hizi ambazo zimedumu kwa miongo kadhaa kwa sababu ya
kuwa na bunge dhaifu lisiloweza kuisimamia serikali kwa dhati hususani
katika mambo makubwa ya kitaifa. Sasa kila hoja inayowasilisha katika
bunge ipewe uzito unaostahili pasipo kujali itikadi ya vyama ambazo kwa
kiasi kikubwa imechangia kwa kashfa hizi kuendelea kudumu kwa miongo
kadhaa” Alisema.
Mambo
mengine ni pamoja na kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo, serikali
kuheshimu misingi ya haki za binadamu, serikali kuheshimu na kulinda
demokrasia pamoja na serikali kuwachukulia hatua watu wote waliohusika
katika miamala ya Tegeta Escrow.
Pia imeitaka serikali kuchukua hatua
katika kashfa zingine ambazo zimesababisha Serikali kupata hasara
ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, kashfa inayohusishwa na Kampuni ya
Lugumi, kashfa ya Richmond, kashfa ya uwepo wa harufu ya rushwa katika
miradi mbalimbali inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii
…mathalani mradi wa NSSF kigamboni pamoja na suala la Vitalu vya
uwindaji na umiliki wake