Hawa ni Baadhi ya Wanawake Wajane walioshiriki katika hafla ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, jana Kigogo-Post Dar es salaam. |
Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wajne Tanzania Wilaya ya
Ubungo Dar es salaam Mh Josephine Chale amemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr.John Magufuli kuwaangalia Wajane kwa jicho la pili ili aone
namnagani anaweza kuwasaidia katika Nyanja ya sheria ambayo itazuia wajane
kuonewa kwa kudhulumiwa haki zao
Chale amewaomba Wajane nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa
Mjane haina maana ndio mwisho wa Maisha,kwani haliya kuwa maisha yanaendelea
Aidha Chale ameushukuru Uongozi wa Msjid Ghadir na Chuo cha
Imam Swadiq kuweza kuwaalika Wajane katika futari ya pamoja ili Wajane wajisikie
kwamba na wenyewe wanatakiwa katika jamii, ili wasijitenge kama vile kwamba
wamefiwa basi ndio maisha yamefika mwisho.
Hayo alisema jana katika halfa ya futari ya pamoja na
Wajane,iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq
Vilivyopo Kigogo Post Dar es salaam.
“Napenda tena kuwashukuru Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo
cha Imam Swadiq kwa kutualika sisi wajane, tumepata faraja kubwa sana, kwani na
sisi tutaenda kufanya kama wanaofanya wenzetu ili tuwape amani wajane.Tunashukuru
sana sana,tunamuomba Mungu awape Moyo wa upendo, awape riziki na awape maisha
marefu.”
Kwa upande wake Mtumishi wa Imam Swadiq Bi.Zaynab Ndete
alisema lengo la hafla hii ya Futari ya Pamoja na Wajane, ni Tumewaalika
wanawake Wajane kutoka Wilaya mbalimbali
za Mkoa wa Dar es salaam, lengo kubwa ni kuzungumza nao na kuwapatia muongozo
wa Kisheria, hususani zinazowahusu wao baada ya kufiwa na waume zao.
“Kwa kweli swala ya Ujane ni swala zito ni swala gumu,
kwasababu ni swala linalomuhusu mwanamke, kama tunavyoangalia katika jamii yetu
ya Kitanzania wajane wengi wanapokuwa wametoza wame zao, wanakuwa ni watu ambao
wanakuwa katika matatizo makubwa sana, miongoni mwa matatizo wanayokumbananayo
ni kutengwa au kunyanyapaliwa na familia ya mume ,kunyang’anywa haki zao za
msingi, kunyang’anywa mali zao ambazo wameachiwa kama urithi na wame zao”
alisema Ndete
“Sisi Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq
tumewaita hapa kwanza kuwasaidia waweze kuzifahamu haki zao, wamama wajane
hawatakiwi wawe wanyonge pale wanapoondokewa na wame zao,kuondokewa na mume ni
jambo Mwenyezimungu (swt) ameliandika kuwa ni lalazima kwani anaweza kuondoka
Mume au Mke” aliongeza Ndete.
“Dini ya Kiislam imesimama kidete juu ya kuwatetea wanawake
wajane, kwani ukiwa mjane unahaki ya Kuishi kama wengine,anahaki ya kuwa na
mali,unahaki ya kuwa Kiongozi,unahaki ya kuwa Bosi, anahaki kuwana amani na
upendo, anahaki ya kuwa Muajiriwa, anahaki ya kuolewa na Mwanaume
mwingine,anahaki ya kumiliki” alisisitiza
Hatahivyo Mtumishi Ndete aliwaomba Wanawake wajane wasiwe
wanyonge na wasimame kidete kuweza kusimamia malezi ya familia zao kwani jukumu
la kuwalea watoto aliokuwachia mumewe iko mikononi mwako.
No comments:
Post a Comment