Monday, March 2, 2015

Sheikh Jalala "Uislam wa Mtume ni Waamani."


Sheikh Hemed Jalala,akisisitiza jambo juu ya Uislam Sahihi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu kilichopo Kigogo-Post, jijini Dar es Salaam amewataka Waislamu kufuatilia Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa Makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali kutoka kwa Wahadhiri.
Hayo ameyasema katika Mhadhara wa Wazi uliokuwa wa siku tatu kuanzia 28, februal, hadi 01-machi 2015, katika viwanja vya Super Sanifu, Round About ya Kigogo, Dar-es -salaam.

Amesema kuwa Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni uislamu wa Amani, kuvumiliana, kupendana, kuheshimiana, kutokukufurishana ,kutodharau dini ya mwenzio na Wenyekukaa Pamoja na watu wenye mtazamo tofauti.


 Aidha ameongeza kuwa Uislamu wa Mtume ni wa amani, huruma na maelewano na kuwa Uislamu halisi utashinda Uislam wa chinja chinja utafeli kwa kuwa unaenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s).



Hatahivyo amewataka watu wote bila kujali dini zao kushikamana na kusikilizana kwani jamii ambayo aina maelewano itakuwa ipo mbali na maendeleo, taifa ambalo linapata maendeleo ni taifa lenye maelewano na mshikamano.

Katika Muhadhara huo uliyomalizika siku ya J.pili ya tarehe 1/03/2015 kulitolewa vitabu mbalimbali vinavyoonesha athari mbaya ya Madhehebu ya Kiwahhabi (ANSWARU SUNNA) Madhehebu ambayo hii leo yamekuwa tishio kubwa kwa jamii ya Kiislamu Ulimwenguni.

Hawzat Imam Swadiq (a.s) Yahimiza Hijab kwa Bint wa Kiislam.

Waschana wenye umri kati ya Miaka 9 hadi 15 wakisoma Duatul Huja baada ya Kupewa mafunzo ya Dini Kiislam, kwa Mnasaba wa kuzaliwa Bibi Zayanab Bint Ali (a.s).

Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala akiwaswaisha kwa Vitendo waschana waliohudhuria katika kusherekea kuzaliwa kwa Bibi Zaynab Bint Ali.
Hawazat Imam Swadiq imesheherekea mazazi ya Bibi Zaynab Bint Ali (a.s)  kwa kuwachukua wasichana 50 wenye umri wa miaka kuanzia 9 hadi 15, pamoja na wazazi wao kwa kuwapatia elimu na mafunzo juu ya Unuhimu wa Hijabu, Swala na sheria zingine za Kiisalamu.

Katika Mafunzo hayo, Samahat Sheikh Hemed Jalala aliwasalisha swala ya jamaa kwa vitendo na kuwataka waschana hao waishi kwa misingi ya Kiislamu,na Wapambike na hijjab kama walivyokuwa Fatma Bint Muhammad (s.a.w.w) na Zaynab Bint Ali (a.s)

Bibi Zainabu Baba yake ni Sayyedina Ali  Ibn Abutwalib (a.s), Mama Yake ni Fatuma Bint Muhammad, Babu yake ni Muhammad Ibn Abdallah na Bibi yake ni Khadija Bint Khuwailid


Sheikh Hemed Jalala akiwapa neno la umuhimu wa Hijab na Ibada zingine kwa bint wa Kiislam.

Waschana wakiwa pamoja na wazazi wao wakiwa makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali

Waschana wa Kiislam wanatakiwa kupambika kwa kuvaa Stara,Ibada, Elimu na Tabia Njema kama alivyokuwa Bibi Zaynab Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)