Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu
ya Lebanon, Hizbullah, amesema anaitazama itikadi ya misimamo mikali ya
Uwahhabi kuwa hatari zaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Sayyed Hassan Nasrallah amenukuliwa na gazeti la Al Akhbar la
Lebanon tolea la Jumanne akisema, "Uwahhabi ni shari zaidi ya Israel,
hasa kwa kuzingatia kuwa lengo la itikadi hiyo ni kuwaangamiza wengine
na kufuta kila kitu kuhusu Uislamu na Historia yake.".
Akihutubu katika hadhara ya wasoma mashairi ya maombolezo, Sayyed
Nasrallah ameashiria kuibuka kundi la kitakfiri la Daesh au ISIS na
kusema: "Mradi huu ulianzishwa mwaka 2011 na si suala la Kisuni na
Kishia. Mashirika ya kijasusi yamehusika na tunapaswa kutumia fursa hii
kukabiliana na Uwahhabi na kuuangamiza." Aidha amesema mgogoro uliopo
hivi sasa si baina ya Shia na Sunni bali ni mgogoro ulioibuliwa na
Mawahhabi.
Ameongeza kuwa, Uwahhabi ni itikadi inayotawala Saudia na inapigiwa
debe na watu wanaopata himaya ya Riyadh ambao wanawavutia magaidi kote
duniani. Amesema magaidi wa ISIS wanatumia itikadi ya Uwahhabi
kuwatuhumu Waislamu wengine kuwa ni makafiri na hivyo kuwaua.
Sayyid Nasrallah ameashiria tishio jingine kubwa zaidi ya Uwahhabi na
Uzayuni kuwa ni 'Ushia wa Uingereza' ambao unafadhiliwa na mashirika ya
kijasusi ya London. Amesema wanaohubiri Ushia huo wanajidai kuwa
wanazuoni wa kidini katika hali ambayo ni mamluki wa mashirika ya
kijasusi ya maadui.
Kiongozi wa Hizbullah amesema hana matumani ya suluhisho la kisiasa
katika mgogoro wa Syria na kuongeza kuwa yanayojiri katika medani ya
vita ndiyo yatakayoamua hatima ya nchi hiyo ya Kkiarabu