Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
ameiomba Serikali ya awamo ya Tano kuenzi misimamo ya Baba wa Taifa katika kuitetea
na kuiunga Mkono jambo la Wapalestina kama ilivyokuwa katika awamu zingine
zilizopita.
“Napenda
Kuiambia na Kuielekeza Serikali yangu Takatifu, Serikali yangu ya Tanzania,
Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali iendelee kuitetea na kuliunga mkono jambo
la Wapalestina kama iliyokuwa Tanzania ya Baba wa Taifa Mwalim Julias Nyerere.”
Alisema Sheikh Jalala
Maulana
Sheikh Jalala alisema hayo jana katika Semina inayozungumzia Mtazamo wa jumla
wa Imam Khomein, ambapo Semina hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa D ini
ya Kiislamu na Dini ya Kikristo, Viongozi wa Serikali, Balozi wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, iliyofanyika Makao
Makuu ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania, Kigogo Post Jijini Dar es salaam.
Aidha Sheikh
Jalala alisema kuwa umoja umoja wetu, amani yetu, maelewano yetu kati ya
Waislamu na Wakristo na utanzania wetu hautakuwa na dhamani kwa binadamu
wengine kama jambo la Wapalestina wataendelea kuishi kwa kudhulumiwa na
kufukuzwa.
“Umoja wetu
Tanzania kati ya Waislamu na Wakristo,
maelewano yetu mazuri tuliokuwa nayo Tanzania, Amani yetu tulionayo Tanzania,
hayoyote hayatakuwa na dhamani kama Wapalestina wataendelea kuishi hali ya
kufukuzwa na hali ya kudhulumiwa na hali ya kunyanganywa”. Alisisitiza Sheikh
Jalala
“Napenda
niseme Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuhusiana na ubaguzi ni dhambi, mtakapo
anza kuwabagua watu mtakwenda kubaguana mpaka mwisho na kuiacha Palestina
ikidhulumiwa katika mazingira yale ni dhambi na dhambi hiyo haitobakia kwa
wapalestina iko siku Wanyamwezi na Wazaramo watafukuzwa katika nchi yao
kutakuwa hakuna mtu wa kuwatetea kwa sababu tuliwaacha wapalestina kule”
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa makini kuandika Nukta Muhimu kutoka kwa Wachangiaji katika semina hiyo. |
Kwa uapande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa
Ibrahimu Lipumba ameitaka Serikali na Watanzania kujifunza kuwa na msimamo wa
kupinga aina yoyote ya dhulma, Ukandamizaji,Unyanyasaji kwa kufuata misimamo ya
Imam Khomein na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
“Imam Khomein alikuwa ni Mtu anapinga Uonevu, unyanyasaji wa
Mtu na nchi yoyote na alikuwa na msimamo madhubuti kuhusu Wapalestinate,Wayahudi,
Waislamu na Wakristo waweze kuishi kwa Amani, hivyo Ni muhimu seriakali ya
awamu ya Tano na Watanzania kwa Ujumla tuweze kuenzi msimamo wa swala la Baba
wa Taifa kuhusu Palestina ambalo katika Msimamo wake Baba wa Taifa unafanana na
msimamo wa Ayatolla Imam Khomein wa kuwaunga Mkono wapalestina waweze kupata
ukombozi katika ardhi yao” alisema Pro. Lipumba