Friday, June 8, 2018

Serikali ya Awamu ya Tano inaombwa kuwatetea Wapalestina


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala (watatu Kulia) akiwa makini kusikiliza wachingiagi wengine katika Semina ya Mtazamo wa Jumla wa Imam Khomein (r.a), Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala ameiomba Serikali ya awamo ya Tano kuenzi misimamo ya Baba wa Taifa katika kuitetea na kuiunga Mkono jambo la Wapalestina kama ilivyokuwa katika awamu zingine zilizopita.
 
“Napenda Kuiambia na Kuielekeza Serikali yangu Takatifu, Serikali yangu ya Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali iendelee kuitetea na kuliunga mkono jambo la Wapalestina kama iliyokuwa Tanzania ya Baba wa Taifa Mwalim Julias Nyerere.” Alisema Sheikh Jalala

Maulana Sheikh Jalala alisema hayo jana katika Semina inayozungumzia Mtazamo wa jumla wa Imam Khomein, ambapo Semina hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa D ini ya Kiislamu na Dini ya Kikristo, Viongozi wa Serikali, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, iliyofanyika Makao Makuu ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania, Kigogo Post Jijini Dar es salaam.
 
Aidha Sheikh Jalala alisema kuwa umoja umoja wetu, amani yetu, maelewano yetu kati ya Waislamu na Wakristo na utanzania wetu hautakuwa na dhamani kwa binadamu wengine kama jambo la Wapalestina wataendelea kuishi kwa kudhulumiwa na kufukuzwa.

“Umoja wetu Tanzania kati ya  Waislamu na Wakristo, maelewano yetu mazuri tuliokuwa nayo Tanzania, Amani yetu tulionayo Tanzania, hayoyote hayatakuwa na dhamani kama Wapalestina wataendelea kuishi hali ya kufukuzwa na hali ya kudhulumiwa na hali ya kunyanganywa”. Alisisitiza Sheikh Jalala

“Napenda niseme Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuhusiana na ubaguzi ni dhambi, mtakapo anza kuwabagua watu mtakwenda kubaguana mpaka mwisho na kuiacha Palestina ikidhulumiwa katika mazingira yale ni dhambi na dhambi hiyo haitobakia kwa wapalestina iko siku Wanyamwezi na Wazaramo watafukuzwa katika nchi yao kutakuwa hakuna mtu wa kuwatetea kwa sababu tuliwaacha wapalestina kule”

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa makini kuandika Nukta Muhimu kutoka kwa Wachangiaji katika semina hiyo.
Kwa uapande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba ameitaka Serikali na Watanzania kujifunza kuwa na msimamo wa kupinga aina yoyote ya dhulma, Ukandamizaji,Unyanyasaji kwa kufuata misimamo ya Imam Khomein na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

“Imam Khomein alikuwa ni Mtu anapinga Uonevu, unyanyasaji wa Mtu na nchi yoyote na alikuwa na msimamo madhubuti kuhusu Wapalestinate,Wayahudi, Waislamu na Wakristo waweze kuishi kwa Amani, hivyo Ni muhimu seriakali ya awamu ya Tano na Watanzania kwa Ujumla tuweze kuenzi msimamo wa swala la Baba wa Taifa kuhusu Palestina ambalo katika Msimamo wake Baba wa Taifa unafanana na msimamo wa Ayatolla Imam Khomein wa kuwaunga Mkono wapalestina waweze kupata ukombozi katika ardhi yao” alisema Pro. Lipumba

No comments: