Sunday, September 20, 2015

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe Nyalandu kuzindua kampeni zake SINGIDA

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, leo anazindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya kutetea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini. Nyalandu, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka 15 sasa, anawania tena nafasi hiyo wakati akiwa na rekodi yenye kujivunia kutokana na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa mafanikio makubwa.  
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Eliah Digha, alisema uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika Kata ya Mtinko jimboni humo. Alisema Nyalandu alichelewa kuzindua kampeni hizo kutokana na kuwa na majukumu mazito ya kichama na kiserikali na kwamba, wananchi walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa siku hii ya leo.  
Digha, ambaye pia ni mgombea udiwani katika Kata ya Msange, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uzinduzi huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni Nyalandu kupanda jukwaani na kuzungumza na wapigakura wake.
“Tunazindua kampeni zetu rasmi leo katika Kata ya Mtinko na baada ya hapo ni nginjanginja mpaka uchaguzi…hatutakuwa na muda wa kusimama hivyo, wapinzani wajiandae kwani hakutakuwa na mapumziko wala mtu kuomba poo. Wametaka kujaribu muziki wa Nyalandu sasa ndio wamewekewa hivyo kama hawajajipanga itakula kwao,” alisema Digha.  
Alisema uzinduzi huo utapambwa na vikundi mbalimbali vya burudani kutoka mkoani Singida na kwamba, shughuli nzima itaanza saa nne asubuhi. Kwa upande wake, Nyalandu alisema atatumia mkutano huo kueleza mafanikio yote yaliyopatikana na mikakati yake mipya ya kuendelea kulivusha jimbo hilo kimaendeleo.
Amesema katika kipindi cha uongozi wake, kwa kushirikiana na wananchi wake wamefanya mambo makubwa kwenye sekta zote muhimu ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii ikiwemo kuwawezesha vijana na akinamama kuanzisha miradi ya ujasiriamali.
 Nyalandu, ambaye ni miongoni mwa makada 32 wanaounda timu ya ushindi ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amesema hana shaka na ushindi mwaka huu.  
Amesema wagombea wa CCM kuanzia wa urais, wabunge na madiwani wataibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na historia ya utendaji kazi itaendelea kuwainua. “Dk. 

Magufuli ana historia ambayo haina utata kuanzia kwenye utendaji kazi hadi uadilifu wake hivyo si wa kufananisha na wagombea wengine kwenye nafasi ya urais. 
Nyalandu anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge akiwa na historia ya kujivunia mbele ya wapigakura wa Singida Kaskazini…vivyo hivyo kwa madiwani wa CCM ambao wanagombea kwa ajili ya kuwatumia watu na si kwa maslahi binafsi kama walivyo wapinzani,” alisema Nyalandu.
Aidha, ametua fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo na kusikiliza mikakati yake mipya kwa ajili ya maendeleo ya Singida Kaskazini.

Soma hapa amechokisema leo Mhe. Mbowe Juu ya NEC na Mgogoro uliopo katika UKAWA

Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo ameitaka Tume ya taifa ya uchaguzi kutoa tamko kuhusu kauli iliyotoleawa na mmoja wa viongozi wa CCM kuwa chama hicho hakipo tayari kuondoka ikulu hata kama kitashindwa katika uchaguzi ujao mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa katika kampeni za Urais mkoani kigoma na mmoja kati ya viongozi wa chama hicho ndugu ABDALA BULEMBO ambapo alisema kuwa hakuna njia inayoweza kuwaondoa ikulu na chama cha mapinduzi hakiwezi kuachia IKULU kwa njia yoyote kauli ambayo imeanza kuibua mijadala mbalimbali nchini Tanzania.

Akizungumza na wanahabari mchana wa leo mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA ndugu FREMAN MBOWE amesema kuwa kauli hiyo imewashtua sana wao kama vyama vya upinzani na kuanza kuwa na wasiwasi kama uchaguzi huo utakuwa na amani kwa kuwa chama chenye serikali kimeapa kufanya njia yoyote ili tu kisiachie ikulu.

Mh MBOWE amesema kuwa kauli hiyo inaweza kuchukuliwa kawaida lakini ni kauli nzito na yenye mafumbo makubwa ambayo yanaweza kusababisha vurugu kubwa na hadi sasa hakuna mtu yoyote wa chama hicho wala tume ya uchaguzi aliyejitokeza kutolea ufafanuzi kauli hiyo.

Amesema kuwa kama kauli hiyo ni kauli ya chama cha mapinduzi ni ukweli kuwa vyama vya upinzani havitaweza kuwa na imani na uchaguzi huo kwa kuwa tayari chama tawala kimesema hakiko tayari kuachia ikulu huku akienda mbali na kusema kuwa kwa kauli hizo hakuna haja ya kuendelea kuwa na uchaguzi ambao chama tawala kinangangania ikulu.

Mh MBOWE amesema sasa UKAWA unaitaka tume ya taifa ya uchaguzi kukitaka chama cha mapinduzi kutolea ufafanuzi kauli hiyo kwani kama ndio kauli yao watangaze kabisa kuwa hakuna uchaguzi kwa kuwa utakuwa ni upotevu wa rasilimali za taifa wakati tayari chama tawala hakiko tayari kukubali matokeo..

MGOGORO WA NCCR MAGEUZI.

Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa chadema amesma kuwa sakata linaloendelea ndani ya chama cha NCCR MAGEUZI ni mwendelezo wa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo kuendelea kufika bei ya kutaka kuisaliti ukawa na hakuna lingine.

Hivi juzi viongozi kadhaa wa chama cha NCCR waliibuka na kudai kuwa chama chao kimekuwa kikiyumba kutokana na mwenyekiti wao kufanya kazi za chadema kuliko za chama huku wakidai kuwa wamekosa majimbo mengi ambayo walikuwa wanayatarajia ambapo Mh mbowe amesema kuwa hiyo sio hoja kwani lengo la UKAWA sio chama kuwa na majimbo mangapi bali ni kuhakikisha kuwa wanaibuka na majimbo mengi bila kujali vyama vyao.

Mh mbowe amesema kuwa swala la mgawanyo wa vyama lilienda sambamba na kuangalia uwezo wa chama husika katika jimbo na kusimamisha mtu ambaye anakubalika katika eneo husika ili kuweza kupata ushindi katika majimbo mengi na sio kutoa majimbo hata kwa watu ambao hawakubaliki katika majimbo hayo.

Serikali Ya Magufuli Kushusha Meli Tano Bahari ya Hindi

wapo mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli atapata ridhaa ya watanzania ya kuunda serikali ya awamu ya tano, serilaki yake itanunua meli tano kubwa zitakazofanya kazi katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Hayo yamesemwa na mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suhuhu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mafia. Aliwahakikishia kuwa serikali ya CCM imejipanga kubadili maisha ya wakazi hao kiuchumi kwa kupitia sekta ya uvuvi.
Aliongeza kuwa ilani ya CCM imeainisha kuwa kila kijiji cha Mafia kitapata shilingi 1,000,000 ili kusaidia kuwainua wananchi hao kiuchumi, fedha hizo zitatumika katika kuwasaidia kununua vyombo vikubwa vya kufanyia shughuli za uvuvi.
Bi. Samia alisema mpango huo umelenga katika kuongeza ajira kwa wananchi wote hususan wakazi wa Mafia.
Kadhalika, alisema kuwa serikali ya CCM imepanga kununua meli nyingine 4 zitakazofanya kazi katika meneo ya Mtwara.
“Mafia mnastahili kuwezeshwa zaidi hasa baada ya kuonesha juhudi zenu kwa kujenga kiwanda cha samki lakini ilani yetu pia inasema tutanunua vyombo kwa ajili ya uvuvi ili kewnda katika ukanda wa kiuchumi wa bahari kuu na kuvua samaki wenye thamani kubwa.”