WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, leo anazindua
rasmi kampeni zake kwa ajili ya kutetea nafasi ya ubunge katika Jimbo la
Singida Kaskazini.
Nyalandu, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka 15 sasa,
anawania tena nafasi hiyo wakati akiwa na rekodi yenye kujivunia
kutokana na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa
mafanikio makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Eliah Digha, alisema uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika Kata ya Mtinko jimboni humo. Alisema Nyalandu alichelewa kuzindua kampeni hizo kutokana na kuwa na majukumu mazito ya kichama na kiserikali na kwamba, wananchi walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa siku hii ya leo.
Digha, ambaye pia ni mgombea udiwani katika Kata ya Msange, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uzinduzi huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni Nyalandu kupanda jukwaani na kuzungumza na wapigakura wake.
“Tunazindua kampeni zetu rasmi leo katika Kata ya Mtinko na baada ya hapo ni nginjanginja mpaka uchaguzi…hatutakuwa na muda wa kusimama hivyo, wapinzani wajiandae kwani hakutakuwa na mapumziko wala mtu kuomba poo. Wametaka kujaribu muziki wa Nyalandu sasa ndio wamewekewa hivyo kama hawajajipanga itakula kwao,” alisema Digha.
Alisema uzinduzi huo utapambwa na vikundi mbalimbali vya burudani kutoka mkoani Singida na kwamba, shughuli nzima itaanza saa nne asubuhi. Kwa upande wake, Nyalandu alisema atatumia mkutano huo kueleza mafanikio yote yaliyopatikana na mikakati yake mipya ya kuendelea kulivusha jimbo hilo kimaendeleo.
Amesema katika kipindi cha uongozi wake, kwa kushirikiana na wananchi wake wamefanya mambo makubwa kwenye sekta zote muhimu ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ustawi wa jamii ikiwemo kuwawezesha vijana na akinamama kuanzisha miradi ya ujasiriamali.
Nyalandu, ambaye ni miongoni mwa makada 32 wanaounda timu ya ushindi ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amesema hana shaka na ushindi mwaka huu.
Amesema wagombea wa CCM kuanzia wa urais, wabunge na madiwani wataibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na historia ya utendaji kazi itaendelea kuwainua. “Dk.
Magufuli ana historia ambayo haina utata kuanzia kwenye utendaji kazi hadi uadilifu wake hivyo si wa kufananisha na wagombea wengine kwenye nafasi ya urais.
Nyalandu anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge akiwa na historia ya kujivunia mbele ya wapigakura wa Singida Kaskazini…vivyo hivyo kwa madiwani wa CCM ambao wanagombea kwa ajili ya kuwatumia watu na si kwa maslahi binafsi kama walivyo wapinzani,” alisema Nyalandu.
Aidha, ametua fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo na kusikiliza mikakati yake mipya kwa ajili ya maendeleo ya Singida Kaskazini.

No comments:
Post a Comment