Mamia ya Waislamu jana walifanya maandamano makubwa mkabala wa Ubalozi
wa Saudi Arabia mjini London, Uingereza wakipinga adhabu ya kifo
iliyotolewa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo dhidi ya Sheikh Nimr
Baqer al Nimr mwanachuoni mashuhuri wa nchini Saudi Arabia.
Waandamanaji hao walipiga nara za 'Mauti kwa utawala wa Aal Saud' na ' Sheikh Nimr aachiliwe huru' sanjari na kubeba mabango na maberamu yaliyo dhidi ya utawala wa kifalme wa Saudi Arabia, walisisitiza juu ya kuachiliwa huru mwanachuoni huyo.
Waandamanji hao sanjari na kuutaja utawala wa Saudi Arabia kuwa mvunjaji mkuu wa haki za binadamu na unayaunga mkono makundi ya kigaidi, wameitaka serikali ya Riyadh kumuachilia huru Sheikh Nimr Baqer al Nimr.
Kijana mmoja wa Kimarekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo amelalamikia jinsi nchi zinazojinadi kuwa watetezi wa haki za binadamu kama vile Marekani na Uingereza kwa kunyamazia kimya hukumu hiyo ya kidhuluma
Na kusisitiza kwamba kimya hicho kinaonyesha wazi kuwepo mashirikiano kati ya madola hayo ya Magharibi kwa utawala huo wa kifalme katika kutenda jinai na kuwakandamiza wananchi wa Saudia. Kijana huyo amesema na hapa tunamnukuu:
' Mimi siyo Muislamu na wala Mwarabu, lakini naamini kwamba Sheikh Nimr ni kiongozi huru ambaye amedhulumiwa na utawala katili na wa kifalme wa Saudi Arabia', mwisho wa kunukuu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yamelaani vikali hukumu hiyo ya kidhuluma iliyotolewa dhidi ya mwanachuoni huyo. Chanzo cha habari:
Sheikh Nimr Baqer al Nimr. |