Thursday, November 9, 2017

Waislamu Nchini waondolewa shaka katika kujiandikisha Sensa

Waislamu watakiwa kumuunga mkono Muft Abubakar kwa kushiriki zoezi la sensa
Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi akizungumza leo Masjid Ghadir, Kigogo Dar es salaam juu ya Umuhimu wa Sensa na kumpongeza Mh. Muft wa Tanzania Abubakar Zuberi.
“Kama umoja wa Vijana wa Kiislamu BAKWATA Taifa tunaomba kuwatoa hofu wale wote ambao wanaoona zoezi la Sensa, kwa Wiaslam linaweza kugeuka kuwa chanzo cha mfarakano wa Taifa Kiimani, haiwezi kuwa hivyo tunavyomfahamu  Mhe. Muft wetu Abubakkar Zuberi ni mwenye kuongozwa na Qur’an na hadith za Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Katibu wa Umoja huo Sheikh Zuberi

Sheikh Zuberi amesema kuwa dhima kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanahesabiwa, makatibu wanapaswa kumsaidia mufti katika hilo ili kuweza kuwa na Idadi kamili ya Wailsamu hapa nchini na kufahamu wako wapi, wanafanya nini, wangapi hawana kazi, wazee wangapi, nguvu kazi ikoje taarifa ambazo ni muhimu kwa mustakabali wa Waislamu.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika eneo la Masjid Al Ghadir Kigogo Post, Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi alisema tangu alipochaguliwa Muft Abubakar mwaka 2015 ameweza kufanya mambo mbalimbali baada ya kutoa maelekezo kwa viongozi wa dini ikiwemo kudumisha amani, kuunganisha jamii,  kuleta maendeleo, ushirikiano mzuri wa Baraza na Mashirika ya Dini ya ndani na nje ya nchi.

Aidha Sheikh Zuberi ameendelea kusema kuwa Mh.Muft kaamrisha mema na kukataza maovu, uboreshaji wa elimu ya dini na secula, kusisitiza kujitambua, mahusiano mazuri kati ya Baraza na viongozi wa nchi, kukataza kufanya kazi kwa mazoea, na sensa kwa maendeleo ya waislamu ambapo ameagiza kupatikana kwa takwimu sahihi kwa waislamu kupitia misikiti mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo Sheikh Zuberi ameongeza kuwa Mh. Muft katika kuonyesha umakini Mkubwa katika kuwatumikia Waislamu, hivi karibuni aliwaagiza makatibu wa Baraza la BAKWATA kujiandaa na Sensa ya waislamu, Misikiti na Madrasa kote nchini, ni zoezi lenye lengo jema la kutoa huduma kwa usahihi kwa watu unaowatumikia.
Waandishi wa Habari, Vijna wa Umoja wa Kiislamu BAKWATA Taifa na baadhi ya wageni waliohudhuria katika kikao hicho kutoka Chuo cha Kiislamu (Hawzat) Imam Jafar Swadiq (a.s) wakifauatilia kwa ukaribu jumbe mbalimbali zinazotolewa na Umoja huo, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es salaam.