Saturday, May 28, 2016

"Serikali wekeni Udhibiti wa Mawasiliano na Teknolojia " Sheikh Ponda


Mwenyekiti wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
Mwenyekiti wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ameitaka Serikali kuweka mikakati Madhubuti itakayosaidia kukua na Kudhibiti kwa Mawasiliano na Teknolojia nchini.

Hayo amesema leo wakati akiongea na Waandishi wa habari katika kongamamno la Viongozi wa Taasisi za Kiislam juu ya Mawaliano kwa teknolojia za Kisasa na Athari zake katika Ukumbi wa Karimje, Dar es salaam.

Sheikh Ponda amesema kuwa Serikali inapaswa kujua Swala la Mawaliano na Teknolojia ni jambo kubwa na lina sehemu kuu mbili ambazo ni huleta manufaa na kuleta madhara katika jamii.

Aidha kwaupande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Dar-Alhijra Morogoro Sheikh Wazir Amani Wamaduga amesema kuwa Mwislam na asie kuwa Mwislam anapaswa kutambua yeye ni sehemu ya Mawasiliano na Teknolojia, hivyo anatakiwa kujua namna sahihi ya kutumia Mawasiliano na Teknolojia hayo.

Hatahivyo Raisi wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania Sheikh Suleimani Kilemile amesema kuwa Uislam ni dini inayoishi na inayokwenda na maisha ya mwanadamu ya kila siku.