Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari punde tu baada ya Swala ya Eid al Fitir, katika Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam. |
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana
Sheikh Hemed Jalala amewataka Watanzania kuwa wakweli, watii, wasikivu, wapenda
amani na wenye kupendana na kuelewana ikiwa ni mwendelezo wa athari
iliyopatiana katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Baada ya kumalizika Mwezi wa Ramadhani tuwe Watanzania
Wakweli, tuwe watanzania wenye Utii, tuwe ni watanzania wenye usikivu, tuwe ni
watanzania wenye kupendana, tuwe ni watanzania wenye kuelewana, hayo yote ni
maelekezo yaliyoko ndani ya Qur’an”
Maulana Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiuongea na
waandishi wa Habari katika kutoa Salamu za kheri na fanaka baada ya Swala ya
Eid al Fitiri, iliyoswaliwa katika Viwanja vya Pipo Kigogo jijini Dar es
salaam.
Aidha Maulana Sheikh Jalala amesema kuwa Tumeona ndani ya
ardhi yetu ya Tanzania ndugu zetu wakristo wakiandaa futari wakiwaalika
waislamu, wakikaa meza moja wachungaji, Maaskofu na Masheikh pamoja na Waislamu
wengine hii ni dalili nzuri yakuonyesha upendo na Mshikamano. Kama tulikuwa
tunakaa waislamu na wakristu tukifuturu pamoja katika mwezi mtukufu wa
Ramadhani, haya ni malezi yanatakikiana yaendelee baada ya mwezi mtukufu wa
Ramadhani”
Mjumbe wa Baraza la Ulamaa wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikh Mulaba Swalehe akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam |
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Ulamaa wa Jumuiya ya
Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Sheikh Mulaba Swalehe amesema kuwa
lengo la Mwezi wa Ramadhani ni watu kuwa Wachamungu utakaopelekea Binadamu
kuishi kwa amani na Salama katika Ulimwengu.
“Leo tunamshukuru Mungu kwa kukamilisha mwezi wa Ramadhani
ambao ulikuwa ni mwezi lengo lake kubwa ni
kufikia Uchamungu, ni wajibu wa kila mmoja kuweza kumsaidia ndugu yake
na kumpenda ndugu yake, kwani kwa hali hii ili tuweze kuishi kwa amani na
salama katika dunia hii.
Mwisho Maulana Sheikh Jalala amesema
kuwa anamuomba Mwenzimungu (swt) upendo tuliokuwanao katika Mwezi wa Ramadhani,
Mahusiano mazuri tuliokuwanayo katika mwezi wa Ramadhani kama watanzania,
mahusiano haya yazidi kuboreka, yazidi kuendelea, utulivu na amani
tuliouonyesha ndani ya Mwezi wa Ramadhani amani hii na utulivu huu namuomba
mwenyezi mungu uendelee katika ardhi ya Tanzania katika masiku mengine, Eid
njema.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakijumuika pamoja na Waislamu wengine duniani katika kushiriki Swala ya Eid al Fitir, katika Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam. |
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiomba dua katika swala ya Eid al Fitir, iliyoswaliwa katika Viwanja vya Pipo jijini Dar es salaam |