Wednesday, October 14, 2015

Umoja wa Ulaya waitaka Urusi kusitisha mashambulio ya anga dhidi ya magaidi nchini Syria

Vikundi vya kigaidi vilivyo na silaha ambavyo vinapinga utawala halali wa Rais wa Syria (Bashar al-Assad), ambao wanaugwa mkono na nchi za Ulaya, Marekani na baadhi ya nchi za kiarabu, ambapo baada ya kuanza mashambulizi ya anga ya Urusi nchini Syria nchi hizo zimedai kuwa wao wanaafiki kushambuliwa kikundi cha kigaidi cha Daesh tu wala si vikundi vingine vya kigaidi ambavyo vinamwenendo wa wastani nchini humo.
Shirika la habari la Ufaransa limetoa taarifa kutoka Luxembourg kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 28 ambao ni wanachama wa umoja wa Ulaya wametoa ujumbe ukisema kuwa: mashambulio ya ndege za Urusi yamevilenga vikundi vyote viliokuwa dhidi ya Serikali ya Syria hata vile viliokuwa na msimamo wa wastani ambavyo viko kinyume na utawala huo, kitu ambacho kinautia hofu umoja huo, hivyo umoja huo umeitaka Urusi kusimasha mashambulizi yake kwa haraka kwa vikundi visikuwa vya Daesh nchini humo.
Wizara ya ulinzi ya Urusi Septemba 29 mwaka huu ziliruhusu ndege zake kufanya mashambulio ya anga kushambulia maeneo ya ngome za vikundi vya kigaidi viliopo nchini Syria hususan kikundi cha Daesh.
Siku kadhaa ziliopita yalifanywa mashambulio makali wakishirikiana kati ya majeshi ya Moscow na Damascus dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini Syria ambapo zilishiriki mashambulio hayo ndige 67 na kupelekea magaidi hao kupata kichapo kikali na kuuwawa idadi kubwa ya magaidi hao nchini Syria.
Hivyo basi utawala wa Marekani, Uingreza, Ufaransa, Ujeruman, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki, nchi zinazounga mkono vikundi vinavyo pinga Serikali ya Syria hivi karibuni wamefanya kikao mjini Ankara na kutoa ujumbe wa pamoja wa kuitaka Urusi kusitisha mashambulio yake haraka iwezekanavyo dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini Syria.chanzo abna

Angalia picha 14 za maonesho yaWatoto ya Sikuu ya Eidil Fitri, Masjid Ghadir, Kigogo-Post, 2015