Kiongozi Mlkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania akitoa salamu za polena rambirambi kwa msiba wa wanafunzi 32 wa lucky Vicent leo Majid Ghadie,Kigogo Post Dar es salaam. |
Kikao na
Waadishi wa Habari, Kimechofanyika leo, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es
salaam, Msiba wa Wanafunzi 32 pamoja na Walimu, Wa shule ya Lucky Vicent,
Mkoani Arusha.
Kwa jina la
Mwenyezimungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu.
Innalilah
Wainna lilah Rajiiun
Sisi sote
tumetoka kwa Mungu na sisi sote mwisho tutarudi kwa Mungu.
“Tumepokea
kwa masikitiko makubwa na kwa huzuni ya hali ya juu, isiyokuwa na kifani, ajali
ya basi ya shule ya Lucky Vicent ya mjini Arusha iliyotokea katika eneo la
mrima Rotia, Karatu na kusababisha vifo vya baadhi ya wanafunzi waiopungua 32
ikiwemo baadhi ya walimu,
Sisi kama
Watumishi wa Imam Swadiq (a.s) makao makuu yapo hapa Kigogo Post Dar es salaam,
sisi kama Waislamu, vilevile sisi kama waislamu wafuasi wa madhehebu ya Shia
Tanzania tunaungana na watanzania wenzetu wote
waslamu na wakristo wanaoishi Tanzania kutoa mkono wa Pole kwa wazazi,
kwa wanafunzi wote waliofiwa,na uongozi mzima wa shule ya Lucky Vicent na
wanafunzi wenzao ambao bado wapo shuleni hapo.
Na vilevile
tunatoa mkono wa pole kwa taifa letu takatifu kwa ujumla na vilevile tonatoa
pole kwa muheshimiwa Raisi wa Taifa hili la Tanzania Dr. John Magufuli.
Napenda
kusema hili limetugusa kwa dhati kama waumini, kama watanzania, kwasababu
tunaposoma katika quran ndio kitabu chetu waislamu, inatuambia yakwamba “Waumini
wote ni ndugu” kwahivyo lililotokea
limewakumba waumini wenzetu,ni wajibu wetu kama watanzania pasia kubaguana kidini,
kiitikadi kimadhehebu,kupendana kuelewana na kuwa pamoja wakati wote waraha
na wakati wa majanga kama hili limetukumba
katika kipindi hiki.
Mtume
Muhammad (s.a.w.w) anaema; hakika sifa ya waumini wanatabia ya kupendana na
kuhudhumiana kama vile unavyoona mwili
mmoja, kiungo kimoja kinapougua na
viuongo vingine vinakesha kwa kuugua haviwezi kubakia salama salmini.
Mwisho Mungu
awape wafiwa subira uvumilivu, na wote waliotangulia mbele ya haki Mungu
wapokee roho zao kwa mikono miwili na awaweke mahala pema ndani ya pepo takatifu, na sisi tuliobakia
hapa nchini Tanzania Mungu atupe upendo, atupe mshikamano, atupe umoja, atupe
kuvumiliana, atupe kuenzi amani na utulivu tuliokuwa nao , Mungu ibariki
Tanzania wabariki watu wake wote
wabariki viongozi wake, amiin amiin amiin,Asateni sana.
Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala